Katibu wa Kamati ya Olympic Taifa.Filbert Bayi akimkabidhi zawadi
mwanariadha Fabian Joseph kwa kushika nafasi ya pili michuano ya Arusha
tourism Marathon.zawadi ya 250,000 |
Afisa Michezo Mkoa wa Arusha.Mwanmvita Okeng'o akimkabidhi zawadi ya
kwanza Angelina Tsere baada ya kushinda Arusha tourism Marathon
alizawadiwa sh 500,000. |
Mratibu wa Tamasha
hilo, Andrea Ngobole katikati akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari awapo pichani
mkurugenzi
wa kampuni ya Arusha Media ambaye ni mmojawapo wa waandaaji wa
tamasha hili Musa Juma katikati akiwa anaongea na waandishi wa habari
kuhusiana na tamasha hilo
Akizungumzia
tamasha hilo na kutaja michezo itakayokuwepo , Mkurugenzi wa Alfredo
Shahanga Sports Promotion ,Alfredo Shahanga katika kati
baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Arusha, Tamasha la Utalii mkoani
Arusha,linatarajiwa kufanyika Januari 28 na 29 kwa kuwashirikisha wanahabari,
wanafunzi wa vyuo na wadau wa utalii mkoa wa
Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alisema, tamasha hilo, ambalo hufanyika
kila mwaka, limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Alfredo Shahanga Sports
promotion..
Alisema awali tamasha hilo, lilipangwa
kufanyika Desemba 27 mwaka 2016 lakini lilisogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa taratibu
za maandalizi.
Ngobole alisema lengo la tamasha hilo ni
kuhamasisha utalii wa ndani na kupinga matukio ya ujangili.
Alisema katika tamasha hilo, kutakuwa na
kongamano la wanahabari kujadili mchango wa vyombo vya habari katika kukuza utalii na kupiga vita ujangili pia sheria mpya ya vyombo
vya habari.
“pia tunatarajia kuwa na maonesho ya bidhaa
za utalii ili kuonesha utajiri wa maliasili zilizopo hapa nchini”alisema.
Mkurugenzi wa taasisi la Alfredo Shahanga promotion, alisema licha ya
makongamano ya masuala ya utalii, pia kutakuwa na burudani na michezo januari
29.
Alisema kutakuwa na mashindano ya riadha ya
Tourism Marathon pia michezo za soka,
kuvuta kamba na ngoma mbali mbali za asili lengo ni kutangaza utalii wa
Tanzania.
“hivi karibuni tutatangaza ratiba ya
mashindano yote, zawadi na wadhamini”alisema.
Hizi ni baadhi ya picha katika tamasha la amani na utalii lililofanyika mwaka 2015 katika viwanja vya general tyre
Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham akimkabidhi
kikombe cha ushindi wa bonanza la amani
na utalii mkoa wa Arusha,nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira lililofanyika vuwanja vya general tyre jijini arusha
Wanamichezo wa kitambinoma wakiwa wanashabikia ushindi mara baada ya
kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha
Post a Comment