PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: VIDEO ya Diamond Yaweka Rekodi Mpya Kenya...Yaongoza Kutazamwa zaidi na Wakenya Youtube
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Video ya wimbo wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Raymond, Salome, ndiyo video ya muziki iliyotazamwa zaidi kwenye mtan...


Video ya wimbo wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Raymond, Salome, ndiyo video ya muziki iliyotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube nchini Kenya, kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, kupitia takwimu ilizozipata.

BBC Swahili wamedai kuwa kwenye orodha ya nyimbo 10 kutoka duniani kote, nyimbo za Tanzania zimetazamwa zaidi. Takwimu hizo zinadhihirisha jinsi ambavyo Wakenya wanapenda muziki wa Bongo Flava kuliko nchi nyingine yoyote ukitoa Tanzania yenyewe.

Hadi sasa, Salome ina views zaidi milioni 9.8 kwenye mtandao wa Youtube.

Hii ni orodha kamili:

Salome – Diamond Platnumz na Raymond
Work – Rihanna na Drake
Bado – Diamond Platnumz na Harmonize
Sauti Sol – Unconditionally Bae, na Alikiba.
Work from Home – Ty Dolla Sign na Fifth Harmony
This is What You Came For – Calvin Harris
Kwetu – Raymond
Cheap Thrills – Sia na Sean Paul
Pillow Talk – Zayn
Ain’t Your Mama – Jennifer Lopez

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top