Mwakilishi wa benki ya NMB akizungumza na wanahabari juu ya udhamini wa semina kwa Tanzania Bloggers Network |
Mwenyekiti wa Tanzania Network Bloggers akizungumza na wanahabari maelezo jijini Daresalaam juu ya semina ya wanachama Tanzania Network Bloggers |
mwakilishi wa NMB akionesha Mfano wa Hundi ya shilingi milioni kumi waliyoitoa kwa TBN kudhamini semina hiyo mbele ya wanahabari |
mwakilishi wa NMB akimkabidhi mfano wa hundi Mwenyekiti wa TBN Joachimu Moshi |
Ndugu
Mwakilishi kutoka Benki ya NMB,
Waandishi
wa habari,
Kwa niaba ya Chama cha
Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network'
(TBN) napenda kuwashukuru kwa kujitokeza katika mkutano huu muhimu. TBN inajua
kuwa mnamajukumu mengi ya kuujuza umma masuala anuai, lakini mmechagua kuja
kwetu ili kutusikiliza tulichowaitia na baadae tunaamini mtaujuza umma juu ya
tukio letu.
TBN iliosajiliwa rasmi
na Serikali mwezi Aprili, 2015 kwa kushirikiana na wataalam wa masuala ya
habari na mitandao ya kijamii imeandaa semina kwa wanahabari hawa wa mitandao
ya kijamii hasa 'Bloggers' itakayofanyika jijini Dar es Salaam. Semina hii
maalumu ambayo itajumuisha mafunzo ya siku mbili yaani tarehe 5 na 6 ya Mwezi
Desemba, 2016 kwa washiriki takribani 150 kutoka Tanzania nzima (Bara na
Visiwani) itafuatiwa na mkutano mkuu kwa wanachama hai wa TBN kujadili masuala
mbalimbali ya chama na tasnia nzima ya mitandao ya jamii.
Ndugu
Wanahabari,
Katika mkusanyiko huu
wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa,
upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya
kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia
kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kama ajira nyingine. Kimsingi lazima tukubali
kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa
muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea
kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.
TBN inaamini njia pekee
ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu
kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au
kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna
atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na
kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii.
TBN inapenda kutoa
shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Nne na Tano chini ya Mh. Rais John Pombe
Magufuli kwa ushirikiano alioanza kuuonesha hasa kwa kutambua mchango wa
mitandao hii ya kijamii na hata kuitumia katika utoaji wa taarifa zao. Kimsingi
hii ni hatua nzuri na ya kuigwa hasa katika ulimwengu huu ambapo dunia imekuwa
kama kijiji kutokana na hatua ya maendeleo ya habari na mawasiliano.
Ndugu
Wanahabari,
Kwa kulitambua hili
mnaweza kuona hata taasisi nyeti kama Ikulu nayo ina Blogu maalumu kwa ajili ya
kutoa taarifa kwa umma, Idara ya Habari Maelezo nayo ina Blogu kwa ajili ya
kutoa taarifa kwa umma juu ya masuala mbalimbali yanayopaswa kutolewa kitaarifa
kwa jamii. Jambo la kujivunia zaidi kwa maendeleo ya mitandao hii hata Waziri
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape M. Nnauye amekuwa
mstari wa mbele kuona umuhimu wa mitandao ya kijamii hasa blogu na hata
kuzitumia katika kupasha habari umma. Hata katika mkutano wetu wa kesho kutwa
ndiye tunayemtarajia kuwa mgeni rasmi atakayetufungulia mkutano huo.
Ndugu
Wanahabari,
Kwa namna ya pekee TBN
inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Benki ya NMB kwa kukubali kuwa wadhamini
wa kuu wa mkushanyiko huo wa 'bloggers' kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa yetu.
Kitendo cha kujitolea kufanikisha jambo hili kinaonesha namna gani NMB
inavyowajali wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo hili la upashanaji
habari kwa jamii.
Kama hiyo haitoshi
tunapenda kuwashukuru wadhamini wengine ambao ni NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola
ambao wamejitolea kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la kuwaleta
pamoja bloggers na kutoa mafunzo kwao. Tunaamini tutakuwa nao siku zote katika
masuala mengi ya maendeleo ya tasnia ya mitandao ya kijamii.
Imetolewa
na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim
E. Mushi
0756469470
Post a Comment