Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye akizungumza na wamiliki wa Mitandao ya Kijamii Bloggers Tanzania (TBN) kabla ya kufunga
mafunzo hayo kwa mablooger hao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
*******************************************
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO- Dar es Salaam
SERIKALI inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa
Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa
waendeshaji wa blog nchini.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za
Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda,
hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Aidha, Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na
makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili
kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi
hivyo makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo
yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.
Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
“Tutumie fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili
kuhakikisha tiunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa
kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania
tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akiwakabidhi baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kadi za uwanachama za
mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSPF katika hafla ya ufungaji wa mafunzo
kwa Bloggers Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wamiuliki wa Bloggers Tanzania wakifuatilia hotuba ya
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa Bloggers Tanzania yaliyofanyika Jijini
Dar es Salaam. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM
Post a Comment