Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kila mtu
duniani ana mwanga ndani yake ama nuru
ya aina fulani ambayo amekuja nayo duniani ili kuiangaza dunia.
Mwanga ulionao ni mithili ya taa ,taa yako inaweza
kuwa kipaji ulichonacho ,ubunifu ama uwezo ulionao ambao unaweza kukutoa kwenye
giza la umasikini.
Wangapi wana
taa ndani yao na bado wanaishi kwenye giza totoro la umasikini,maradhi na ujinga.
Pengine una
taa ndani yako ila hujui namna ya kuiwasha ili ujiangazie na kuwaangazia
wengine ndio maana uko gizani.
Gundua taa
yako ni ipi,itumie kujimulikia na kuwamulikia wengine ili utoke
gizani,umezaliwa kung`ara na si kukaa gizani.
Wengine wana
taa ambazo zinapaswa kuwamulikia wengine na kwa kutokujua wamesababisha giza
kwenye maisha ya watu wengi.
Ni vizuri
kutumia taa yako kuwamulikia wengine usiweke taa yako chini ya kitanda maana
haitakua na manufaa kwako wala kwa jamii yako.
Iweke taa
yako juu ya kinara sehemu iliyoinuka ili
iweze kuwaangazia wengine kwani taa hiyo itakua na umuhimu tofauti na ile
iliyowekwa uvunguni mwa kitanda.
Nikiwa
Chuoni Mwalimu wangu aliniambia ukiona taa inawaka kwenye nyumba ya jirani usiipige mawe kwani inaweza kukuangazia na
kuwaangazia wengine walioko mbali.
Nilijifunza
kutowapiga vita,majungu watu wenye taa nikiamini kuwa kuna siku naweza
kunufaika na taa hizo zikiwaka zinaweza kuniangazia na mimi.
Kila mtu
kwenye maisha anatamani kung`ara kufanikiwa lakini tatizo hawajui kutumia
kutumia mwanga ,taa walizonazo ama kuziweka mafuta ili ziweze kuangaza zaidi.
Wako ambao
walishindwa kuweka taa zao mafuta zikazima,vipaji vikazima jambo ambalo ni
hatari kwenye maisha ya kila siku.
Pia kuna
baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa wakizima taa za wenzao taa zao zitawaka
zaidi na kuonekana jambo ambalo sai kweli,kila mtu atang`aa kwa mwanga wake
(shine with your own light) .
Kila mtu
amezaliwa ang`ae kila mahali alipokusudiwa
kung`aa na aliyekuumba ,iwe ni kiuchumi,kifamilia,sanaa ,filamu n.k .
Ang`ae kwa
kile alichonacho ndani yake ndicho kitamfanya ang`are mpaka kuwashangaza watu
na kufurahiwa,kuwa maarufu na kufanikiwa sana kutokana na kile ulichonacho.
Inuka
Uangaze
0765938008
Post a Comment