Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gariya polisi mara baada ya kulazimika kwenda
mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na
kuwekewa na pinganizi la dhamana
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gariya polisi mara baada ya kulazimika kwenda
mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na
kuwekewa na pinganizi la dhamana
mke wa mbunge wa jimbo la Arusha mjini
Neema Lema akiwa anaondoka mahakamani kumsindikiza mme wake mara baada
ya mahakama kuisha na lema kuamriwa kwenda mahabusu ya magereza hadi
ijumaa ambapo kesi yake itatajwa tena
Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema ambaye alishtakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali, leo November 8 amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha na kusomewa shtaka linalomkabili baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba.
Hakimu
mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi anayesikiliza kesi hiyo Desdery
Kamugisha amesema hawezi kutolea maamuzi kwenye mahakama hiyo kwa kuwa
anahitaji muda wakusoma na kupitia vifungu vya sheria na hoja
zilizotolewa na November 11 atatoa maamuzi.
Kutokana
na hatua hiyo Godbless Lema amerudishwa mahabusu hadi November 11 mwaka
huu. Wakili wa Chadema John Malya amesema kutokana na hoja zote
zilizowasilishwa kwa pande zote mbili zimeonekana zina uzito hivyo
wanasubiri uamuzi wa mahakama.
Post a Comment