Waziri wa Maliasili na
Utalii Profesa Jumanne Maghembe
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya Utalii mkoani Arusha
unaotarajiwa kufanyika kesho.
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari ofisini
kwake,amesema kuwa mkutano kama huo ulifanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2012
hivyo wameona ni vyema serikali kushirikiana na wadau wa utalii kukaa pamoja
kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili
ili kuboresha sekta hiyo,ambayo asilimia 80% ya watalii wanaoingia
nchini hufika mkoani hapa .
Amesema kuwa mkoa wa Arusha ni kitovu cha cha utalii na
unachangia pato la mkoa kwa asilimia20% na kitaifa kwa asilimia 17%ambapo mwaka
2015 idadi ya watalii iliyoingia nchini ilikuwa 1,137,182 na kuingizia Taifa
kiasi cha dola za kimarekani 1.9 milioni,katikaq idadi hiyo asilimia 80%watalii
walitembelea mkoa kwasababu ya vivutio
vingi vilivyopo mkoani Arusha.
Amesema kwamba madhumuni ya mkutano huo ni kujadili hali ya
maendeleo ya utalii ya mkoa ,fursa zilizopo,mafanikio ,changamoto na kuweka
mikakati yakuboresha huduma mbalimbali za utalii ambapo wadau watapata fursa ya
kubadilishana mawazo na kuadhimisha siku ya utalii duiaani amabayo huadhimishwa
kila mwaka septemba 27.
“Maadhimisho haya ya utalii mwaka huu yamebeba kauli mbiu UTALII KWA
WOTE,Kwa kuzingatia hilo wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya utalii zikiwemo
TANAPA,NCAA,HAT,TTB,TATO,TTGA, TRA,TACTO Watawasilisjha mada ambazo zitalenga
kuboresha utalii,pamoja na kuhakikisha elimu na fursa za Utalii zinaifikia
jamiii “ alisisitiza Gambo.
Amesema kuwa wadau watakaoshiriki mkutano huo ni wahifadhi,Wakala
wa waongozaji watalii,Wakala wa wausafirishaji watalii,watoa huduma za malazi,Bodi
ya Utalii,na Viongozi watendaji wa serikali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Waziri wa maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe.
Mkutano huo wa siku moja umefadhiliwa na Shirika la Hifadhi
la Taifa (TANAPA)kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na
Ofisi ya Kanda ya Utalii ndiyo waandaaji wa mkutano huo wa wadau mbalimbali wa
Utalii Mkoani Arusha.
Post a Comment