PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DC SAME AAGIZA NAKALA ZA VIKAO VYOTE VYA WODC WILAYANI HUMO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA: ISMON MJEMA, SAME: Serikali Wilayani Same imeagiza kupewa nakala ya vikao vyote vya Serikali   Wilayani hapo,kuanzia ngazi ya ...
Image result for MKUU WA WILAYA YA SAME ROSEMARY SENYAMULE

NA: ISMON MJEMA, SAME:
Serikali Wilayani Same imeagiza kupewa nakala ya vikao vyote vya Serikali  Wilayani hapo,kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata (WODC) hadi Halmashauri ili kufuatilia  kwa ukaribu utekelezwaji wa agizo la kufanya vikao vya kisheria,ikiwemo ufuatiliaji wa utekelezaji wa Muhtasari wa vikao husika.

Akizungumza na Baraza la Wazee Kata ya Suji,mara baada ya kumaliza kushiriki katika Msaragambo wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Malindi na Kituo cha Afya cha Kata hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule,nakala zote za vikao vya Serikali zinazopelekwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri,zipelekwe Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili Ofisi hiyo iweze kufuatilia vikao hivyo kwa ukaribu zaidi;Ikiwemo kuona Tija inayotokana na Vikao hivyo.( 201 609 053 15 16-DC)

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wazee Kata ya Suji wameusifu uamuzi wa Mkuu huyo wa Wilaya,kwa kutaka nakala za vikao Serikali vya kisheria kwa kudai kuwa itaongeza ufanisi wa utekelezaji wa maazimio ya vikao.

Vijiji kadhaa nchini, Serikali za Vijiji hivyo zimekuwa zikituhumiwa kutokusoma mapato na matumizi na kutokufanya vikao halali vya kisheria na wananchi,hali ambayo imekuwa ikiwaacha wananchi njia panda wakiwa na maswali yasiyo na majibu na kupelekea Watu kutokuwa na Imani na Viongozi wao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top