Familia
ya Ankal Muhidin Issa Michuzi inapenda kutoa shukrani nyingi sana
sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa
kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae
Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki
iliyopita na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
juzi Jumamosi.
Ni
vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa
jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na
baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe
tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo
tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie
mko wengi mno.
Pamoja
na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma
Kikwete na familia yao yote, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali
Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee
Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri
Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu
Kiongozi Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo,
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue pamoja na wafanyakazi
wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na
kuhakikisha kuwa kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa.
TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...
Salamu
zingine za kipekee ziwaendee watumishi wote wa Ubalozi wetu Afrika
kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na
Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha
mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE
MTAPOPUNGUKIWA...
Vile
vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya
Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo
Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa
na unasafirishwa kwa heshima zote. ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...
Kwa
Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia
inatoa shukurani za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na
mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa
watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa
magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba mfiwa Ankal ni mwanachama.
Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family
Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG),
Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New
Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in
Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN),
The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi,
Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, RUBY 15,
Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi
Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na Jamii
Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA
KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA,
SANA, SANA...
Mwisho,
lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani
za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa
mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa
kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Dar es salaam.
HATUNA
CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA
KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU
ZOTE...
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un
AMIN!
Post a Comment