PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA YA UCHUMI: DEGREE /DIPLOMA SIYO KAZI SEHEMU YA I
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA ADSON KAGIYE     Katika pitapita zangu nakutana na vijana we...



https://lh6.googleusercontent.com/-xIpjgqv2UcA/AAAAAAAAAAI/AAAAAAAAAAA/F_1A0MyWG1s/s128-c-k/photo.jpg 

NA ADSON KAGIYE


 
Katika pitapita zangu nakutana na vijana wengi wasio na kazi na kisha huwa narudi nyuma kuchunguza maisha yangu ya Chuo na ya shuleni. Naangalia jamaa zangu wengi tuliomaliza nao chuo, secondari na shule ya msingi. Unakuta kuna jambo moja wazi linalotenganisha waliofanikiwa na wasio fanikiwa,makala hii itakuwa ndefu lakini kwa leo ebu tuangalie msaada wa degree yako ktk kufanikiwa.
Nakumbuka siku najaza form kujiunga BBA enzi hizo lengo ilikuwa ni kuweza kuja kupata kazi na kuingia BOT.. Sikujua yatakayojiri nitakapokuwa chuoni wala yatakayojiri baada ya kumaliza Chuo, nayo ni long story.
Kuna kundi kama 3 hivi za wanaojiunga Chuo
1. Wanaotaka degree/diploma ili wapate Kazi za ajira, kupanda cheo, daraja, mshahara na pia kuendeleza taasisi binafsi au project zao
2. Wanaotaka degree/diploma ili kuendekeza vipaji vyao - hawa ni wachache sana
3. Wanaotaka DEGREE/DIPLOMA tu liwalo na liwe.. Yaani fashionist
HOFU YANGU IPO KATIKA KUNDI LA 3 NA SEHEMU KUBWA YA GROUP 1.
Kuna vijana wengi hawana kazi mtaani, ukiwachunguza vizuri unakuta ni walewale wa kozi zilezile za vyuo vilevile. Na hapa ndio unajiuliza hawa walikuwa na lengo lipi tangu mwanzo.. Je akiwa shuleni hakuona watu wa coz hizo wakihangaika? Au DEGREE IMEKUWA FASHIONI?
ILI MADA HII IWEZE KUENDELEA CHANGIA KWA KUJIBU MASWALI YA MJADALA YAFUATAYO
Unadhani kwa nini wanachuo wakimaliza wanakosa kazi za ajira au za kujiajiri ile hali wana ELIMU?
Majibu
A. Hawana ujuzi na uzoefu
B. Walichagua coz vibaya
C. Uzembe
D. Hawana refarii wa kuwapatia kazi au sponsor wa shughuli zao za biashara
C. Hawana mitaji
E. Hawakufaulu vizuri
E. Hawana network ya kuweza kuwapa taarifa kama kazi zipo wapi, mitaji IPO wapi, masoko yapo wapi nakadhalika
F. Sijui
Andika jibu lako kwa mtindo huu.kwenye comment box Ukianza na sababu unayoona ni kubwa zaidi na kumalizia na sababu ndogo..
Mfano
B
D
E
A
MAKALA HII INAENDELEA..............

Na.Adson Kagiye

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top