Kituo
cha Mikutano cha KimataifaArusha (AICC)kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo
la upungufu wa madawati katika mkoa huo.
Akipokea
madawati hayo jijini Arusha jana, Ntibenda amesema kwamba msaada huo ni sehemu ya
juhudi za serikali mkoani Arusha kuwashirikisha
wadau wa maendeleo ili kuhakikisha shule
zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.
“Napenda
niishukuru sana AICC kupitia kwa Mkurugenzi Mwendeshaji Elishilia Kaaya kwa kuitikia
vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa
wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Alitoa
wito kwa wadau
mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wafanyakazi
wa ofisi ya Mkoa wa Arusha nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha
kila mwanafunzi ana kaa katika dawati.
Akizungumza
baada ya kukabidhi madawati hayo, Afisa Mwandamizi waItifakina Uhusiano wa AICC, Catherine Kilinda amesema kwamba AICC
kama shirika la umma linawajibu wakuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha
sekta ya elimu hapa nchini.
“Sisi
kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara tunaona fahari kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzaia wa kuhakikisha watoto
wetu wa shule hawakai chini na ndio maana
leo hii tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga
mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua
sekta ya elimu”, alieleza Catherine.
Post a Comment