Ni kweli kabisa, kuna watu wengi walio na kazi lakini
hawana Elimu, Leo hii si jambo la kushangaa kuona kampuni kubwa ina HR
wa kike aliyeishia form four lakini secretary wake ni diploma. Juzi tu
tumeona Waziri akiwa na diploma lakini wasaidiz wake wana PhD.
Hata wazazi wetu walifanya kazi mbalimbali za mikono na
kisha kutusomesha, wengine humu wamesomeshwa na maziwa tu, wengine
kahawa, wengine, mbao, wengine viazi, wengine sukari. Wazazi hawa hata
siku moja hawakusema 'ETI HATUNA KAZI' na kukaa kuilalamikia serikali,
BADALA YAKE WALIKAZANA NA KAZI ZAO ZA MIKONO in fact walijua hawawezi
pata KAZI za ajira kwa kuwa hawakusoma. Siku hizi hata mlinzi lazima uwe
form four na cheti cha mgambo.
Mfumo wa Elimu Tanzania hasa elimu isiyo ya ufundi au
udaktari, hauandai 'KAZI' unaandaa 'AJIRA' na hapa ndio penye tatizo,
kwa kuwa unapomaliza Chuo na degree/diploma ya sociology, habari, ualim
nk jamii inakutegemea uwe na kazi ya ajira au ya kujiajiri. But ukiingia
mtaani kuna watu kibao wanaohitaji ushauri wa kijamii, kindoa, kisheria
na kidini, KOSA UNALOFANYA UNASOMA TU sociology vitabuni bila
kujiongeza. UKIMALIZA CHUO unajikuta huna ujuzi wowote wa kupata kazi ya
ajira au kujiajiri.
Hata waliosoma masomo ya biashara hujikuta hawawezi hata
kuandika mpango wa biashara wa Kuku. Hawa walisomo ili kuajiriwa ktk
kampuni za wengine.
Na hapa ndipo thamani halisi ya degree yako inapojulikana.
Mfumo huu mbovu umerithishwa toka wakoloni, na imekuwa ngumu kubadilika.
Unaposikia mtoto wa miaka 10 Finland amegundua tatizo ktk
mtandao wa kijamii wa Facebook usidhanie ni kitu cha kubahatisha, mfumo
wa shule unamruhusu kuwa curious.
SASA HIVI UPO SHULE MATHALANI HUONI TOFAUTI SANA. LAKINI
UKISHAMALIZA SHULE NDIO UTAANZA KUONA TOFAUTI NA KUJIULIZA THAMAN YA
DEGREE/DIPLOMA YANGU IPO WAPI.
Binafsi huwa napingana sana na wanaoilaumu serikali kwa kukosa kazi kwao, huwa nawauliza. JE FURSA HAKUNA?
KAMA ZIPO KWA NINI MIMI NIPATE WEWE UKOSE?
Na ndio mada ya Leo
Katika mahali ulipo
''JE FURSA ZIPO AU HAZIPO NA KAMA ZIPO JE UNAWEZA ZIPATA''?
Chagua linalokufaa
A. Fursa Zipo na naweza zipata
B. Fursa zipo but zinavipingamizi
C. Fursa Hazipo
D. Sijui
Chagua jibu moja TU!
Na....Mr.Adson Kagiye
Na....Mr.Adson Kagiye
Post a Comment