Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen
Mbazi Msuya (katikati) akifuatilia bajeti ya Idara yake pamoja na wataalamu
wake kushoto kwake ni Charles Msangi na kulia ni Daniel Alfei wakati wa kikao
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya
Kupitisha Bajeti Aprili 12, 2016.
(Picha
Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza Idara
ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya tathimini ya hali halisi za
athari zilizosababishwa na ndege aina ya kwerea kwerea katika mashamba ya mtama
na uwele yaliyopo Mkoani Dodoma katika Wilaya Bahi.
Waziri Mhagama aliyasema hayo
wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha Kupitisha
Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kiliibua hoja za
wajumbe ikiwemo hoja iliyo bainisha athari za maafa kwa wakazi wa Wilaya ya
Bahi kuhusu ukosefu wa chakula baada ya mashamba yao kuvamiwa na ndege
waharibifu aina ya Kwerea kwerea.
Hoja hiyo iliibuliwa na Mbunge wa
Bahi Bw. Omar Badwel alisema wananchi wake wapo katika wakati mgumu hivyo
wanahitaji msaada kutoka serikalini kwa kuwa mazao yao yamevamiwa na ndege hao.
“Kwerea kwerea wamekuwa ni changamoto kwa
wakazi wa wilaya yangu hususani maeneo ya Manyoni ninaomba serikali kupitia
Idara ya Maafa isaidie kwa kuwapa chakula na mbegu Wananchi ili waweze kujikimu
na kuitatua changamoto hiyo”Alisema Badwel.
“Mazao yaliyoshambuliwa na
kuharibiwa na ndege aina ya kwerea kwerea ni mazao ya mtama na uwele,
Alisisitiza”.
Waziri Mhagama alisema anatafuta
uwezekano wa kuona umuhimu wa kushirikisha Wizara ya kilimo na Mifugo kwa
kuangalia namna zinavyoweza kushirikiana kuondoa wadudu waharibifu wa mazao
mkoani Dodoma.
“Serikali itafanya tathmini kwa
waathirika hao wa maafa Wilayani Bahi, ni vizuri Idara ya Maafa ifanye hivyo
haraka ili kusaidia kunusuru hali ya wakazi wa Dodoma”Alisisitiza Mhagama.
Waziri Mhagama alimpongeza Mhe.Badwel kwa kuwajali
wananchi wa Bahi kwa kuibua jambo muhimu hivyo aliahidi kulitafutia ufumbuzi wa
haraka.
“Suala hili ni muhimu kwa kuwa
linagusa maisha ya Wananchi moja kwa moja sisi kama serikali tumelichukua kwa uzito na
tutahakikisha Idara ya maafa inatembelea maeneo husika kwa ajili ya
kufanya tathimini za haraka kwa
waathirika waliopoteza mazao yao ili kujua namna tunavyoweza kutoa msaada wa
haraka katika maeneo husika ” alisema Mhagama.
Awali;
kikao hicho kililenga kupitia na kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
yenye fungu namba 25 (Ofisi Binafsi ya Mhe.Waziri Mkuu), 37(Sera, Uratibu a
Bunge), 15 na 65 (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) na fungu 27 na 61 (Tume
ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi.
|
Post a Comment