Ntibenda alitoa amri hiyo ofisini kwake wakati akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa yote ya jiji la Arusha.
Alisema hataweza kuvumilia makanisa hayo kuzinduliwa kila mahali katika makazi ya watu na kufanya ibada usiku kucha.
"Mimi ni mkristo, sikatazi waumini kusali, lakini nataka kuwe na utaratibu maalumu, sio kila kukicha unakuta kanisa jipya na kibaya zaidi yanasumbua hata wageni wanaoingia jijini hapa." Alisema Ntibenda.
Kutokana na kauli hiyo ya mkuu wa mkoa, Askofu Mkuu wa Kanisa na Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amejitokeza hadharani kupinga kauli hiyo.
Gwajima amesema Tanzania ni nchi huru, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, kila mtu ana haki ya kuabudu muda wowote na wakati wowote atakao bila kuingiliwa na mtu yeyote.
Amesema waumini wa makanisa ya kilokole Tanzania wako zaidi ya milioni 11, hivyo kuwazuia kuabudu ni sawa na kutafuta matatizo mengine
Gwajima amesema waumini wa Kiislam huamka saa kumi usiku kuswali kwa sauti kubwa na hakuna mtu huwaingilia kwa kuwa hiyo ni haki yao kikatiba.
Post a Comment