Na. Mwandishi Maalum
Ofisi ya Waziri Mkuu imewasilisha Utekelezaji wa Miradi mitatu
inayoiratibu kwa Kamati ya Bunge na Sheria; Miradi hiyo ni Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za
Kifedha Vijijini Mradi wa Taarifa za Hali ya Hewa na Uboreshaji wa Mifumo
wa Taadhali za Awali pamoja na Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Nchi katika
kujiandaa na kukabiliana na maafa.
Akitoa ufafanuzi wa
miradi hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) kwa Kamati hiyo ya Bunge
Machi 31, 2016 ilipokutana na Ofisi ya Waziri Mkuu, alibainisha kuwa miradi
hiyo inalenga kupunguza umasikini na kujenga uwezo wa Serikali katika
Menejimenti ya Maafa
Mhagama alifafanua kuwa
Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha
Vijijini Mradi niya miaka saba ambayo utekelezaji wake ulianza mwaka 2011,
lengo la programu hiyo ni kufanikisha adhima ya serikali ya kupunguza umasikini
na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwezesha kaya za vijijini
kujiongeza kipato na usalama wa chakula
"Programu
itafanikisha malengo yake kwa kuboresha miundo mbinu ya masoko, kuongeza
thamani mazao ya kilimo, kupanua wigo wa huduma za kifedha zipatikanazo
vijijini na kuwajengea wananchi waishio vijijini uwezo wa kuyafikia
masoko"alisema Mhagama
Kwa upande wa Mradi
wa Taarifa za Hali ya Hewa na Uboreshaji wa Mifumo ya Taadhali za Awali
alibainisha kuwa, mradi huo unalenga kuimarisha uwezo wa nchi katika kukusanya
takwimu za hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi yanayoweza kusababisha
maafa.
"Pia mradi
utasaidoia kuboresha mifumo ya utoaji wa taarifa za awali ili kuzuia au
kuhimili athari za majanga yanayoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabia
nchi".Alisisitiza
Aliongeza kuwa
Kuimarisha Uwezo wa Nchi katika kujiandaa na kukabiliana na maafa unalenga
kuongeza uwezo wa Serikali na Taasisi zake katika Menejimenti ya Maafa na
kuboresha ufanisi wa Mamlaka za Serikali za mitaa katika kujiandaa na
kukabiliana na maafa.
Makamu Mwenyekiti
wa
Kamati hiyo mhe. Najma Giga (mb) alibainisha kuwa wameridhishwa na
utekelezaji wa miradi hiyo, na kupendekeza kuwa miradi hiyo iongeza
nguvu Vijijini katika utekelezaji wake ili iweze kuwafikia wananchi
wengi zaidi.
Post a Comment