Mapumziko ya Rais John Magufuli nyumbani
kwao, Chato mkoa wa Geita, yanaonekana kuwapasua vichwa viongozi wa
serikali ya mkoa huo kutokana na kutoelewa ratiba yake kwa muda
atakaokuwapo nyumbani hapo.
Rais Magufuli aliwasili juzi mjini Chato
akitumia usafiri wa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
iliyotanguliwa na helikopta ya polisi, kabla ya kuwahutubia wananchi wa
wilaya hiyo.
Ujio huo ni wa kwanza tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba 25, mwaka jana.
Hata hivyo, Nipashe jana ililazimika
kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, ili kufahamu
ratiba ya shughuli atakazofanya Rais Magufuli muda atakaokuwapo hapo.
Hata hivyo, hali hiyo imeonekana pasua
kichwa kwa viongozi hao, baada ya mkuu wa wilaya kudai tangu Rais
awasili nyumbani kwake, viongozi hao walielekezwa kuendelea na majukumu
yao ya kawaida.
"Ukweli viongozi hatuna ratiba yoyote
zaidi ya mapumziko, maana tangu amewasili nyumbani tulielezwa kuendelea
na kazi zetu za kawaida na Rais atakapotaka kufanya jambo atatujulisha
kupitia kwa mkuu wa mkoa,” alisema Ntarambe.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli
juzi aliwapongeza wananchi wa Chato kwa kujitokeza kumsikiliza kwenye
mkutano wake wa hadhara, licha ya kuchelewa kutoa taarifa za ujio wake
kwa kuwa hakupenda kupokewa kwa kishindo kwa sababu huko ni nyumbani
kwao.
Nawapongeza kwa kunipokea. Najua wengi
mmepata taarifa za ujio wangu kuanzia jana (juzi) saa 11. sikupenda
kupokewa maana nakuja nyumbani, ndiyo maana kila napogeuka hapa nawaona
wazee wangu mpo hapa wengi," alisema.
Post a Comment