Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Watu wengi hutumia muda wao baada ya kazi kukaa na
marafiki,makundi rika na wengine hufanya mambo ambayo huwazuia kuzifikia ndoto
zao.
Wengine
hutumia muda wao baada ya kazi kuongeza vipato vyao kwa kufanya miradi binafsi
,kuongeza maarifa kwa kujisomea vitabu na majarida mbalimbali ,kuhudhuria
semina,mafunzo na makongamano.
Muda
unaoutumia baada ya kazi unaweza kukuongezea mafanikio au kukupunguzia
mafanikio yako katika maisha.
Muda
unaotumia baada ya kazi unaweza kukuongezea maisha au kukupunguzia maisha
kulingana na yale unayoyafanya.
Simaanishi
uwe bize masaa 24 hapa naongelea yale masaa kadhaa baada ya kazi ambayo watu
huyatumia kujiachia ,kujistarehesha,kujipumzisha baada ya kazi jambo ambalo ni zuri si vibaya
.
Muda huo
watu wengine huutumia kufanya maongezi ambayo ni hasi huyaharibu mafanikio yao
na kuwazuia kuingia kwenye mafanikio yao.
Baada ya
kazi kuna vitu vingi unaweza kuvifanya ambavyo unavipenda kama vile kujifunza
ala za muziki,kujisomea kuongeza maarifa maana bila maarifa watu huangamia hata
kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa “watu
wangu huangamia kwa kukosa maarifa”.
Tunapaswa
kujijengea tabia ya kutafuta maarifa kwa kujisomea ,kusikiliza ,video,sauti
ambazo zinakupa maarifa ya kujenga familia,jamii na taifa.
Watu wengi
hukosa muda wa kujitafuta wewe ni nani?,kwanini
uko duniani?,unapaswa kufanya nini? Pia kujitafakari na kujitathmini
wamezidiwa na mbio za maisha ,kazi na marafiki hivyo kujikuta akikimbizana na
kazi na kuacha kukimbiza ndoto zake.
Kuwa na
mwendo wa kasi katika maisha ni kitu muhimu lakini kwenda kasi bila kuwa na
mwelekeo si kitu,weka dira yako ama mwelekeo wako kadiria mbio zako kisha kimbilia
ndoto zako mpaka uzifikie.
Wengine
hujikuta wakitafuta furaha maishani mwao
na kujikuta wakikimbizana na furaha kwa kudhani kuwa wakipata kitu Fulani
watakua na furaha wanakipata hicho lakini bado hawapati utoshelevu ndani yao.Wanatafuta vitu vingi wanavipata au kuvikosa lakini hawapati furaha
ya kutosheleza .
Hatujui ya
kuwa furaha haitokani na wingi au uchache wa vitu ulivyonavyo,furaha ya kweli ni kuwa na amani
ya kweli na kuridhika na vile ulivyonavyo haijalishi na vingi au vichache.
Watu wengi
hufanya kazi masaa machache huku wakitumia masaa mengi kujipumzisha ,kupiga
zogo,kujistarehesha ,kutembea na marafiki,makundi yasiyofaa ndio maana
mafanikio kwao yanabaki kuwa ndoto.
Ndege wanaofanana huruka pamoja,Nakutakia
mafanikio katika maisha yako
0765938008
Post a Comment