Mwongozo
wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2016/17 umeandaliwa kwa kuzingatia
Kifungu Na. 21 cha Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015. Aidha,
Mwongozo wa Mpango na Bajeti wa Mwaka 2016/17 umejikita katika kujenga
Taifa lenye uchumi wa viwanda kama ilivyoainishwa kwenye Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 pamoja na Mpango Elekezi wa
Miaka 15.
Warsha
hiyo ambayo imeandaliwa na ushirikino wa mashirika matano ambayo ni
Oxfam, Policy Forum, ANASAF, Action Aid na TGNP zaidi ikiwa ni kuwaleta
pamoja wakulima hao wadogowadogo katika kupitia mwongozo na kuujadili
kwa ukaribu pamoja na kuuchambua kwa kina zaidi.
Wakati
akitoa majumuisho kutoka ukurasa wa 14-20 Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa
wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo ameomba Mkulima ameiunga mkono hoja
ya mwanamke kuthaminiwa na kupata nafasi ya kuuza Bidhaa zake, kupewa
nafasi ya kujitambua na kumiliki Ardhi, huku akiulalamikia mwongozo huo
wa bajeti elekezi kutoweka wazi kuhusu mfuko wa wanawake katika kusaidia
uzalishaji na kuomba bajeti inayokuja izingatie hilo.
Mzee
Namagono Hassan kutoka kundi la wakulima ametoa maelezo kutoka ukurasa
wa 6-9 kuhusu mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17, kuwa
pamoja na kuanzishwa kwa Benki ya wanawake, isitazame tuu wanawake wa
mjini bali na vijijini kwani wao ndio wazalishaji zaidi wa Chakula
kuliko waishio mijini.
Kwa
upande wake Datius Pastory Inshansha Mwanaharakati na Mkulima mdogo
ukurasa wa 20-23 amepitia ukurasa 23-24 unaotoa maelekezo mahsusi kwa
sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa na kushauri kuwepo
uwazi wa mapato na matumizi ya Serikali za Mitaa, pia Bajeti ielekezwe
zaidi vijijini kulipo mjini na kudhibiti fedha za uvuvi,kilimo na
ufugaji zisiishie kwa watu wachache bali wahusika kwa ujumla.
Maelezo
mengine yametolewa na Bwana Adam Simwinga kuhusu ukurasa wa 9-15
kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti kwamba amegundua hakuna
mkakati wa kuongeza mapato kupitia simu, mkakati wa msamaha wa kodi,
hivyo wameshauri kilimo kiwe ni sehemu ya eneo wezeshi na malighali
katika viwanda nchini Tanzania na katika mpango wa maendeleo na kuongeza
kuwa asilimia 30% hazijitoshelezi kukuza sekta ya kilimo nchini.
Wanaharakati
hao wameishauri serikali kutowasahau katika kuwawezesha mikopo ili
kukuza sekta zao kimaendeleo huku wakilalamika wakulima kutoshirikishwa
kikamilifu.
“Tunaomba
mkopo wa Magari ya wabunge upungue kutoka Mil 90 hadi Mil 20 ili zile
mil 70 zitumike katika shughuli zingine za maendeleo ikiwemo na kilimo
na pia kuwe na viwanda vidogo vidogo katika mikoa mbalimbali mfano
kiwanda cha Machungwa” aliongeza Bi. Kidani Mhenga wanajadili ukurasa wa
3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti.
Bi
Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo akitoa
majumuisho kutoka kipengele cha namna ya kudhibiti Bajeti za Serikali
kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka
2016/2017 ukurasa wa 14-20, picha ya juu ni wanakundi wakiwa wanajadili
swala hilo. Picha ya juu ni baadhi ya mama Shujaa wa chakula ambao
wanatoka katika Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Tanzania pamoja
na wadai wengine wa kilimo .
Mzee
Namagono Hassan Kutoka kikundi namba moja akitoa maelezo kutoka katika
mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017
kutoka ukurasa wa 6-9 unaoelezea mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti
2016/17.
Datius
Pastory Inshansha ambaye ni Mwanaharakati na Mkulima mdogo mdogo
akiwasilisha kundi lake la Tano ambao walikuwa wanajadili ukurasa wa
20-23 kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa
Mwaka 2016/2017 inayozungumzia maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za
mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa.
Bwana
Adam Simwinga akitoa maelezo kutoka kundi namba mbili ambao walikuwa
wachambua mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 ukurasa wa
9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti.
Bi.
Kidani Mhenga kutoka kikundi namba tatu ambao walikuwa wanajadili
ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti za Serikali
kuoka katika mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017.
Baadhi ya wakulima, wafugaji na wavuvi wakiendelea namjadala
Post a Comment