PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: OFISI YA WAZIRI MKUU-YASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhag...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kikao cha Kamati hiyo Februari 11, 2016 kilichofanyika Ukumbi wa Millenium Tower Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe.  Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika tarehe 11 Februari, 2016 Ukumbi wa Ngorongoro Millenium Tower Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka akichangia hoja kuhusu uwepo wa mifuko ya hifadhi za jamii wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika Februari 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji (katikati) akifungua kikao kilichohudhuliwa na wajumbe Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na wabunge walio kwenye kamati hiyo Februari 11, 2016 katika Ukumbi wa Ngorongoro Millenium Tower Makumbusho Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Bw.Eric Shitindi akielezea muundo wa Ofisi ya Waziri Mkuu na majukumu yake wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika Ukumbi wa Ngorongoro Millenium Tower Februari 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Naibu Waziri(watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika Februari 11, 2016 Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top