|
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini makabidhiano hayo yalifanyika jana .
|
|
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa magodoro kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini makabidhiano hayo yalifanyika jana .
|
|
Magodoro waliyokabidhi tigo ikiwa ni ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .
|
Wafanyakazi wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana
|
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (kushoto) , ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .
Iringa, Februari 17, 2016:
Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye
thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika wodi za
Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi kukosa sehemu za kulala, mkoani
Iringa.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya
kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida.
“Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa
pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi
katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema Kiswaga
Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na
mashuka 35.
Mvua zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba
zilisababisha watu 1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya
watu yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa
mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza.
Msaada kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango
wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi
ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia
jamii majanga yanapo ibuka.
|
Post a Comment