Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Watu wengi
duniani wanasumbuliwa na tatizo la kutokujua kwanini wapo duniani na wanatakiwa
wafanye nini?
Wamejikuta
wanafanya kazi ili walipe bili na kulipa kodi
bila kujua kuwa maana ya maisha haishii kwenye kulipa bili ya
umeme,maji,ada na kodi ya pango.Maana ya maisha inakwenda mbele zaidi ya hapo
na haina mipaka ya namna hiyo.
Wako watu
wanaofanya kazi ambazo hawazipendi na wanaenda kazini kila siku na kurudi
nyumbani jioni ama usiku wamechoka huku wakiwapa mgongo wenzi wao wakati wa
usiku kutokana na msongo wa mawazo,stress,maumivu na machungu waliyonayo
wanashindwa kufurahia maisha.
Yote hayo ni
Kwasababu wanafikiri wanaishi ili kulipa bili na kodi mbalimbali hawaoni cha zaidi
katika maisha yao.
Matokeo yake
wamejikuta wamekua watumwa wa fedha ,fedha zinawatumikisha mpaka mpaka
wanasahau kuzitumikia ndoto zao na kutimiza kusudi la maisha yao.
Matajiri wengi hawafanyi kazi kwa
ajili ya fedha,fedha zinafanya kazi kwa ajili yao na kuwazalishia fedha hivyo
hana haja ya kutafuta fedha kwa sababu amejenga miundombinu za fedha hivyo
fedha zinaflow kumfuata yeye na si yeye anazifuata.
Tengeneza
mazingira ya kuzitumikisha fedha zikusaidie kutimiza ndoto zako ,maono na
mawazo mazuri uliyonayo na si kuishia kufurahia kuwa unaweza kulipa bili na
kodi bila kusumbuliwa.
Katika moja
ya makala zangu nimewahi kuandika juu ya mvuto alionao mtu ambao unavuta fedha
mithili ya sumaku fulani hivi,kwa maana ya kipaji,ubunifu na uwezo wa kipekee ambao
unahitajika unaweza kuutoa ukabadilishana na watu wa kakupatia fedha.
Kwa maana
fedha hupatikana kwa nguvu ya mbadilishano aidha bidhaa kwa fedha ama huduma
kwa fedha ,na kila mtu amezaliwa ana bidhaa ama huduma iko ndani yake ambayo ni
muhimu sana kwa jamii akianza kuitoa nje itahitajika na watu watamletea fedha
wapate huduma yake.
Fedha
zinakupenda na sio wewe unazipenda katika vitabu vitakataifu imeandikwa kwamba “Ukipenda sana fedha hutashiba fedha” pia imeandikwa “Mali ikiongezeka na walaji wanaongezeka “ kwa maana fahari ya
tajiri inaweza kuishia kwenye macho yake wala asifahidi kwa kiwango stahiki.
Ni vizuri
kuwa tajiri lakini ni vyema kuwa tajiri anayetimiza kusudi la maisha yake
,haina maana mtu kuwa na fedha nyingi alafu anaishi maisha ambayo hayana maana
wala sababu.
Baada ya
kupata fedha nyingi,jumba la kifahari na magari bado kuna swali linakujia
kwanini uko duniani ilo ni swali la muhimu ambalo unapaswa kulijibu ili
kutimiza kusudi la wewe kuwepo duniani na kuishi maisha yenye maana.
Ina maana
gani kuishi maisha ambayo hayana maana ? ina maana gani kuwepo duniani na
kutokujua sababu ya kuwepo duniani?
Tafakari
chukua hatua.
0765938008
Post a Comment