Wakati
akikanusha vikali taarifa mbaya za kuzushiwa kifo mwishoni mwa wiki
iliyopita na watu ambao alisema hajui lengo lao, habari ya heri ni
kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani)
anaelezwa kuwa kwenye shamrashamra za ndoa baada ya kudaiwa kulipiwa
mahari na mfanyabiashara maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa
sasa).
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu, hivi
karibuni mrembo huyo alilipiwa mahari hayo kwa siri kwa kuwa mwanaume
huyo hakutaka mambo hayo yafike kwenye vyombo vya habari.
“Sasa mimi nawapa habari motomoto kuwa
Lulu amelipiwa mahari na mwanaume wake wa sasa lakini ishu nzima
ilikuwa kwa siri sana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Shughuli nzima ilifanyika nyumbani
kwa Lulu (Mbezi-Beach, Dar) na sasa kinachoendelea ni taratibu za harusi
lakini jamaa (huyo mwanaume) hataki iwe na mbwembwe.
“Ndiyo
maana Lulu sasa hivi ametulia siyo kawaida yake. Hata kwenye viwanja
vya bata na shughuli za mastaa haonekani kwa sababu anafanya mazoezi ya
kukaa nyumbani kama mke wa mtu.”
Habari
hizo zilidai kwamba, Lulu ataolewa ‘soon’ kwani maandalizi yamepamba
moto kimyakimya chini ya usimamizi wa mama yake, Lucresia Karugila.
Baada
ya kunyaka madai hayo, Amani lilizungumza na Lulu ili kumpongeza kwa
kuchumbiwa na kulipiwa mahari kisha kusikia neno lake juu ya ishu hiyo
ambapo tofauti na matarajio ya mwanahabari wetu, msanii huyo
alikasirishwa na habari hizo huku akiweka wazi kuwa mambo mengine katika
maisha yake ni ya binafsi na kwamba siyo kila kitu anaweka wazi kwa
watu wengine.
“Hayo
ni mambo binafsi, kwenye maisha yangu siyo kila kitu cha kuweka wazi
kwa watu,” alisema Lulu kisha akakata simu kwa hasira.
Chanzo:GPL
Post a Comment