MKURUGENZI wa mafunzo wa chuo cha uandishi wa habari Arusha Bwana Joseph mayagila akifundisha somo la ujasiriamali kwa waandishi wa habari mkoani Arusha hivi karibuni |
hapa mkurugenzi huyo akiwa na mkewe mara baada ya kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wakiana mama wa kanisa la TAG sanawari mkoani Arusha |
Kufanikiwa kifedha ni jambo jema na pia ni haki yako ya kiasili ambayo unayo ili uweze kutawala mambo na kutiisha mambo hapa duniani. Hii ni kwasababu kuna mambo ambayo hutaweza kuyatawala wala kuyatiisha hapa duniani mpaka tu pale utakapokuwa umefanikiwa kifedha! Hata hivyo, kufanikiwa kifedha hakujileti kwenyewe, bali ni kitu cha kufanyia kazi, tena chenye wajibu mkubwa unaodai bidii na maarifa kwa kiwango kikubwa. Watu wajinga peke yao, hudhani kufanikiwa kifedha ni bahati ya mtu na kwamba si kitu kinachohitaji mipango! Je unaweza kuvuma maisha ambayo hajayapanda?
Kufanikiwa kifedha kunadai rasilimali!
Kufanikiwa kifedha kunadai kwanza kukuza rasilimali za kichwani mwako kabla ya rasilimali zingine. Duniani kuna rasilimali za aina mbalimbali kama vile rasilimali watu, mali asili yaani ‘natura resources’, rasilimali za kijamii (social resource: ndugu,mila na desturi nzuri ), rasilimali muda na rasilimali za kiroho(spiritual resources), nakadhalika.
Lakini kama unataka kufanikiwa kifedha rasilimali ya kwanza, ambayo utaitumia kuvuta rasilimali zingine ni “mental resources” yaani rasilimali za kichwani mwako. Jambo la uhakika ni kwamba, hata kama ungekuwa unaishi kwenye kijiji ambacho ardhi yake ni dhahabu , na mito yake ni nishati ya mafuta, lakini kama ukishindwa kukuza rasilimali za kichwani mwako, utaendelea kuwa maskini.
Hii ni kwasababu rasilimali za kichwani(maarifa) ndiyo rasilimali kiongozi katika uchumi. Kwa mfano, kuna nchi ambazo duniani hazifugi mifugo kama ng’ombe, mbuzi au farasi, lakini ndiyo zinazoongoza duniani kwa kutengeneza na kuuza viatu vya ngozi. Zipo pia nchi ambazo hazina misitu, lakini ndiyo zinazoongoza duniani kwa kutengeneza na kuuza fenicha na magogo. Je unafikili ni kwanini?
Sisi hapa nchini kwa mfano, ni nchi ya tatu Afrika kwa kuwa na mifugo mingi, yaani ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku, lakini hatuna hata kiwanda kimoja cha kutengeneza viatu ambavyo vinaongoza sokoni kitaifa, au kimataifa. Wala hatuongozi kwa kuuza maziwa au nyama Afrika. Na wala hatuongozi kwa kunywa maziwa kwa uwingi, au kula nyama na mayai, na watoto wa nchi hii bado wanasumbuliwa na utapiamlo. Je unafikiri ni kwa nini?
Je nifanyeje ili nikuze rasilimali zangu za kichwani?
Wahenga waliwahi kunena “Maendeleo yoyote ni matokeo ya hali njema iliyojengwa katika fikra za mtu au watu furani kwa wakati furani, yaani “Any development, is a result of a particular state of mind.” Neno “state of mind” humaanisha hali ya ufahamu, au hali ya uelewa, au mtazamo. Hapa inamaanisha kuwa kuna kiwango cha fikra ambacho unatakiwa kukifikia ili uweze kufanikiwa ipasavyo kiuchumi.
Kwa hiyo, jambo la kwanza kama unataka kukuza rasilimali za kichwani mwako kwa kiwango cha juu unahitaji mafunzo ya namna ya kufanywa upya nia au macho ya kiakiri ” kugeuzwa’ au kujigundua kwamba wewe unawito gani wa kufanikiwa kiuchumi. Yaani, ni shughuli gani kuu ambayo ukiifanya maisha yako ya kiuchumi yatabadilika kabisa kabisa na wewe kuwa mtu mwingine kihistoria? Je wito wako wa kufanikiwa ni kwa kufanya nini hapa duniani? Je wewe una vinasaba(DNA) vya kufanya shughuli gani kuu kiuchumi? Kumbuka hukuumbwa ili ufanye kila kitu, Mungu peke yake ndiye kila kitu!
Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji cha Arusha Journalism Training College (AJTC) kilichoko kwa Mrombo Arusha. Makala haya ni sehemu ya Mafundisho yaliyomo katika vitabu vyake vinne alivyoviandika ambavyo ni “Fanikiwa Kibiashara”, “Jinsi ya kuwa Tajiri”, “Kubuni Biashara Ikupasayo” na “Je fedha zako ni mbegu au mavuno?”.Vitabu hivi vinapatikana kwa shilingi elfu kumi kwa kila kitabu kimoja. Kama unahitaji vitabu wasiliana nasi 0716 20 15 85 au 0763 20 15 85 au whatsap 0715 76 96 15.
SHARE MAKALA HII NA MARAFIKI ZAKO WENGINE!
Post a Comment