MKURUGENZI
na Mmiliki wa Blog ya Wananchi Le Mutuzi amezindua rasmi shamrashamra
za sherehe za kuazimisha miaka mitata ya blog hii hivi punde jijini Dar
es Salaam na kusema kuwa kuelekea siku rasmi ya sherehe hizo kesho
kutakuwa na Semina ya vijana waliomaliza vyuo vikuu lakini
hawajafanikiwa kupata kazi au kujiajiri.
Le
Mutuzi ambaye pia ni 'KING OF ALL SOCIAL MEDIA' kama anavyofahamika
,amesema kuwa katika semina hiyo itakayofanyika katika ukumbi ulipo
jengo la Golden Jubilee TOWER ,vijana watakao hudhuria katika Semina
hiyo watapata fursa ya kukutana na kuzungumza na wafanyabiashara vijana
,wanasaisa na watu mbalimbali waliofanikiwa kimaisha kama njia ya
kuwajengea vijana hao uwezo.
Aidha
amesema kuwa Siku ya jumamosi ambayo itakuwa siku rasmi ya sherehe za
kutimiza miaka mitatu ya BLOG YA WANANCHI,sherehe hizo zitafanyika
katika hoteli ya KILIMANJARO KEMPISKI huku bendi ya THT ikitumbuiza
katika tukio hilo.
Pia
Le Mutuzi ametoa wito kwa vijana wote nchini ambao wamenmaliza vyuo
kufika katika Semina ya kujengewa uwezo wa kujiajiri ili kupunguza wimbi
la vijana wasio na ajira nchini.
Awali
akizungumza,Le Mutuzi amefichua kuwa alianza kazi ya BLOG miaka mitatau
iliyopita huku akiwa na mtaji wa dola 500 ambazo alizitumia kununua
laptop ambayo hadi hii leo ipo na inafanya kazi .
Post a Comment