Afisa
Mahusiano wa Mo Dewji Foundation, Zainul Mzige (wa pili kulia)
akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 100 kwa Mwenyekiti wa
mradi ufugaji kuku wa kienyeji katika kijiji cha Msoga, Michael Mkindo
(wa tatu kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya ya
Bagamoyo, Mh. Majid Mwanga (kushoto) na Diwani wa kata ya Msoga, Hassan
Mwinyikondo (kulia).
Afisa
Mahusiano wa MO Dewji Foundation, Zainul Mzige akisoma hotuba wakati wa
makabidhiano ya mfano wa hundi kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji chotara
kutoka kijiji cha Msoga, Chalince mkoa wa Pwani. Wa kwanza kushoto ni
mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Chalinze, Majid Mwanga, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Msoga,
Hassan Mwinyikondo.
Mfuko
wa MO Dewji umeupatia mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara wa
kijiji cha Msoga mkoani Pwani shilingi milioni 100 kufanikisha
uendeshaji wa mradi huo awamu ya kwanza.
Mradi
huo unaokisiwa kuwa na makisio ya uzalishaji ya sh 2,777,901,500
ulibuniwa mwaka 2013 kwa lengo la kukabiliana na umaskini kijijini hapo.
Kwa
mujibu wa taarifa za mradi makisio ya mapato kutokana na mauzo ya
mayai, vifaranga na kuku baada ya kukoma kutaga zinakadiriwa kuwa sh
4,913,708,000
Aidha mradi huu unasimamiwa na kufadhiliwa na rais Mstaafu Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Akikabidhi
hundi hiyo ya sh milioni 100, Afisa Mahusiano wa Mo Dewji Foundation,
Zainul Mzige alisema kwamba fedha hizo zitaumika kujenga mabanda 200,
ununuzi wa vifaranga, ununuzi wa chakula cha kuku, chanjo na dawa na
malipo kwa wataalamu.
Afisa
Mahusiano wa MO Dewji Foundation, Zainul Mzige akisoma hotuba wakati wa
makabidhiano ya mfano wa hundi kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji chotara
kutoka kijiji cha Msoga.
Mambo mengine ni utawala, mawasiliano, ununuzi wa chachu za mpunga na vifaa vya chakula na maji.
Mzige
alisema pamoja na kutoa fedha hizo kuunga mkono juhudi za Msoga Poultry
Farming Project (MPFP) kuendesha na kuuendeleza mradi kibiashara,
aliwataka wahisaniwa kutambua kwamba maendeleo ya mradi wao yatategemea
sana namna wanavyokuwa makini kutumia fursa mbalimbali kujiimarisha.
Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita Mo Dewji Foundation imetumia zaidi
ya dola za Marekani milioni 3 kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya
kijamii nchini.
Aidha hivi karibuni Mfuko wa MO Dewji kwa kushirikiana na kampuni ya Darecha Limited walizindua shindano la Mo Mjasiriamali lenye lengo la kusaidia kukuza ujasirimali miongoni mwa vijana.
Shindano ya Mo Mjasiriamali
litatoa fursa ya ukuzaji wa mitaji, ulezi wa wajasiriamali na mitandao
ya biashara kuongeza mwanga, ujasiri na kuzalisha wajasiriamali
Tanzania.
Ili
kufanikisha nia ya kuwa na wajasiriamali wengi, shindano hilo
linatarajiwa kuwa daraja kwenda kwa Ofisa Mtendaji, Mohammed Dewji (MeTL
Group na mwenyekiti wa Mo DewjiFoundation) ambapo vijana ambao
wanaonekana wana kitu cha kufanya, lakini hawana msaada watashiriki kwa
lengo la kupata msaada katika mfumo wa mtaji, mtandao na usimamizi wa
ukuaji wa shughuli wanayofanya au kutaka kuifanya ili kuianzisha na
kuikuza.
Kwa
niaba ya wananchi wa Msoga, mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete
alimshukuru Mwenyekiti wa Taasisi ya Mo Dewji, Mohammed Dewji kw
ufadhili ambao ameufanya kwa wananchi wa kijiji cha Msogo na kumtaka
kuwa na moyo wa kutoa zaidi ili azidi kusaidia wananchi walio na
mahitaji.
Mbunge
wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani kwa MO Dewji
Foundation mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 100 kwa
ajili ya ufugaji wa kuku wa kienyeji Chotara.
Alisema
kuwa kupitia mradi huo wa ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara, wananchi
wa kijiji cha Msoga wataweza kujikwamua na janga la umasikini na
wataendelea kuwa wakiandika maombi ya miradi mbalimbali ambayo wanataka
kuifanya ili kuzidi kutengeza ajira zaidi kwa wananchi wa Mzoga.
“Tunamshukuru
Mohammed Dewji kwa msaada huu tunaimani utasaidia wananchi wa Mzoga na
namuomba asisite kutupokea muda mwingine tunapokuwa na miradi mingine,”
alisema Kikwete.
Nae
Mratibu wa Mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara (Msoga Poultry
Farming Project), Novatus Kailembo alisema wazo la kuanzisha mradi huo
lilitolewa na Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete mwaka 2013 ili
kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wa Msoga kama kiuchumi, kielimu na
kiafya.
Alisema
wanataraji kuanza na wanakijiji 300 ukiwa ni mradi wa mfano, awamu ya
kwanza ambao wanataraji kuanza kufanyika katika vitongoji tisa ambavyo
ni Hospital, Takalagame, Kota, Mnazi Mmoja, Tumbi Juu, Tumbi Chini,
Kingugi, Mkundi na Mokela.
Mkuu
wa Wilaya ya Chalinze, Majid Mwanga akimshukuru Mwenyekiti wa MO Dewji
Foundation, Mohammed Dewji kwa ufadhili ambao ameutoa kwa wilaya yake
kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara ambapo ufugaji huo
unataraji kufanyika katika kijiji cha Msoga.
Post a Comment