PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: KUELEKEA MIAKA 3 YA BLOG YA WANANCHI;MKURUGENZI WA BLOG HIIYO LE MUTUZI NATION ASEMA HAYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MKURUGENZI na Mmiliki wa Blog ya Wananchi Le Mutuzi amezindua rasmi shamrashamra za sherehe za kuazimisha miaka mitata ya bl...


MKURUGENZI na Mmiliki wa Blog ya Wananchi Le Mutuzi amezindua rasmi shamrashamra za sherehe za kuazimisha miaka mitata ya blog hii hivi punde jijini Dar es Salaam na kusema kuwa kuelekea siku rasmi ya sherehe hizo kesho kutakuwa na Semina ya vijana waliomaliza vyuo vikuu lakini hawajafanikiwa kupata kazi au kujiajiri.


Le Mutuzi ambaye pia ni 'KING OF ALL SOCIAL MEDIA' kama anavyofahamika ,amesema kuwa katika semina hiyo itakayofanyika katika ukumbi ulipo jengo la Golden Jubilee TOWER ,vijana watakao hudhuria katika Semina hiyo watapata fursa ya kukutana na kuzungumza na wafanyabiashara vijana ,wanasaisa na watu mbalimbali waliofanikiwa kimaisha kama njia ya kuwajengea vijana hao uwezo.


Aidha amesema kuwa Siku ya jumamosi ambayo itakuwa siku rasmi ya sherehe za kutimiza miaka mitatu ya BLOG YA WANANCHI,sherehe hizo zitafanyika katika hoteli ya KILIMANJARO KEMPISKI  huku bendi ya THT ikitumbuiza katika tukio hilo.

Pia Le Mutuzi ametoa wito kwa vijana wote nchini ambao wamenmaliza vyuo kufika katika Semina ya kujengewa uwezo wa kujiajiri ili kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira nchini.

Awali akizungumza,Le Mutuzi amefichua kuwa alianza kazi ya BLOG miaka mitatau iliyopita huku akiwa na mtaji wa dola 500 ambazo alizitumia kununua laptop ambayo hadi hii leo ipo na inafanya kazi .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top