Mamlaka ya MawasilianoTanzania TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika, Kiss Fm na Uhuru FM kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati ..
Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano
wa TCRA Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa
ifikapo kesho saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa
madeni yanayowakabili.
Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha
pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu
haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA na mteja.
Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka wadau wote wa
mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku
akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.
==> Vituo vingine vilivyofungiwa ni;
Sibuka FM, Breez FM, Country FM, Ebony FM, Hot FM, Impact FM, Iringa Municipal TV Kiss FM Kitulo FM Kifimbo FM Mbeya City Municipal TV Radio 5 Radio Free Afrika (RFA) Musa Television NetworkPride FM radio Radio Huruma Radio Uhuru Star TV Rock FM RadioStandard FM radioSumbawanga Municipal TVTanga City TV Top Radio FM limited Ulanga FM

Post a Comment