Wakati
baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali wa burudani nchini wakiendelea
kuwa na hofu juu ya mfumo mpya unaovitaka vituo vya redio na runinga
kuwalipa wasanii mirahaba inayotokana na kucheza kazi zao, serikali
imesema imeunda sheria ambayo itavifanya vishindwe kuepuka kucheza
nyimbo za wasanii wa ndani.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa filamu ya ‘Home Coming’ Mlimani City jijini Dar es
Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye
alisema sheria hiyo inazitaka TV na Redio zenye vipindi vya burudani
kuhakikisha 60% ya content ni ya nyumbani.
“Tumeshatangaza kuanzia tarehe moja mwezi wa kwanza 2016 kila muziki wa msanii utakaopigwa kwenye redio ma television utalipiwa.
"Sheria
ilishasainiwa na tumekubaliana na watu wa COSOTA wataisimamia na
tumeweka kampuni ya kusimamia muziki umepiga mara ngapi na TV gani.
“Mimi
nataka watu waniamini historia yangu, waamini watu watalipwa na haki
yao wataipata na jasho lao watalipata. Nilichowaambia kila jambo jipya
lazima litakuwa na mapungufu ila sheria ndio zitatuongoza, kila redio na
TV zenye vipindi vya burudani wanatakiwa kuhakikisha 60% ya content
wanayoitoa iwe ya nyumbani, hakuna wakukwepa hili,” alisisitiza Nape.
Pia Nape alisema tayari ameshakaa na wahusika wa nyombo vya habari na kuzungumzia namna ya utekelezaji wa suala hilo.
“Vyombo
vya habari ndio wamekuwa wakinisukuma kufanya hivyo, kwahiyo kama wao
ndio wameamua hivyo sisi ulikuwa ni utekelezaji na naamini kila kitu
kitaenda sawa.”
Post a Comment