Pichani ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence
Milanzi ambaye leo ameapishwa rasmi kuanza kupambana na majangili ambao
wamekuwa kero kwa nchi hii.
Ikumbukwe kuwa kuna wakati Tanzania ilifikia kuwa kinara cha matukio ya
ujangili kiasi cha Serikali ya Awamu ya Nne kuanzisha Operesheni
Tokomeza ambayo nayo haikuisha vizuri.
Maliasili ya Tanzania ikitunzwa vizuri inaweza kuwa chanzo kikuu cha
mapato kwa nchi ambayo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa
uchumi kupitia utalii.
Tunakutakia kila la heri katika majukumu yako mapya Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Post a Comment