Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwasili katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4,
2016.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea idara mbalimbali za
hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi.
Baadhi
ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na Kitengo cha
dharura, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la
dawa la MSD na kukagua ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.
Akizungumzia
ziara hiyo mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla
ameeleza kuwa ili kuweza kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika
hospitali hiyo ya taifa tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
alipofanya ziara ya kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa
hospitali hiyo hali iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia
hospitali.
Dk.
Kingwangalla alisema amefurahishwa na utoaji wa huduma katika upimaji
kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI ambazo awali wakati wanaingia
madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya ufanyaji wa kazi na kuwataka
watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuifanya hospitali
hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa hospitali ya taifa.
Alisema
limekuwa jambo ambalo linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika
hospitali ya taifa zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali
za watu binafsi na akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa
Muhimbili kuwa hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi
wananchi wenye uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda
hospitalini hapo.
“Ni
jambo la kushangaza hospitali za watu binafsi zinakuwa na watu wengi
kuliko hapa na wakati sisi tuna madaktari bingwa zaidi ya 500 hapa
Muhimbili lakini hizo hospitali zao hazina hata daktari mmoja bingwa
lakini na huduma zinazopatikana katika madaraja ya juu zinatakiwa
kuboreshwa,
“Kama
tunaweza kuwa na huduma nzuri katika first class (daraja la kwanza)
tunaweza kuwavuta wananchi wengi waje hapa na waache kwenda hospitali
binafsi, wanatakiwa kutengwa madaraja ya juu ambayo huduma zake zinakuwa
zimeboreshwa sio mtu anakuwa daraja la kwanza alafu bado anachangia
choo na wengine au anaelala nae hapewi kitanda,” alisema Mhe.
Kingwangalla.
Aidha
Mhe. Dkt.Kingwangalla aliwatupia lawama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) kwa jinsi wanavyopanga madaraja ya hospitali na kuilinganisha
Muhimbili na hospitali zingine za watu binafsi kuwa jambo hilo siyo
sahihi kwa kuiweka hospitali ya taifa sawa na hospitali za watu binafsi.
“NHIF
wanaweka sehemu moja hospitali ya taifa na hospitali binafsi hili
haliwezekani walinganishe huduma zilizopo hospitali ya taifa na zile
zingine, nina mpango wa kuwatembelea hivi karibuni nitazungumza nao,”
alisema Kingwangalla.
Aidha
Mhe. Naibu Waziri aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuongeza
vitanda katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo awali ilikuwa na
vitanda sita hali ambayo ilikuwa ikiwashangaza wananchi wengi kutokana
na kuwepo kwa vitanda zaidi ya 1350 katika hospitali hiyo na hivyo
kuongezeka kwa vitanda katika wodi hiyo kutasaidia upatikanaji wa wa
huduma bora kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Awali
akitoa taarifa mbele ya Mhe. Dkt. Kingwangalla, Mkuu wa Idara ya Mionzi
katika hospitali hiyo, Dkt. Flora Rwakatare alisema tangu kuanza kwa
kutumika kwa mashine ya MRI mwishoni kwa mwezi Novemba mwaka jana jumla
ya wagonjwa 560 wamefanyiwa vipimo katika mashine hiyo na ndani ya siku
tatu amabazo wamefunga mashine mpya ya CT-Scan wameshawapima wagonjwa
26.
Alisema
kufungwa kwa mashine ya CT-Scan kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya
kwa watanzania kutokana na kasi ya ufanyaji kazi kwa mashine hiyo ambayo
imetengenezwa na kampuni ya Siemens ambayo inauwezo wa kupima kifua na
tumbo kwa sekunde 6.
“Mashine
ya CT-Scan ambayo imefungwa ina ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa
Afrika Mashariki na kwasasa tunategemea kufanya kazi kwa ubora zaidi
kutokana na ukubwa iliyonayo na inaweza kufanya kazi kwa kasi tofauti na
ile iliyokuwa ikitumika awali,” alisema Dkt. Flora.
Nae
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence
Mseru alisema awali hawakuwa wakifanya visingizo ili wasifanye kazi
lakini ni hali halisi iliyokuwepo kuwa mashine iliyokuwepo awali ilikuwa
na matatizo lakini kufanikisha kufungwa kwa mashine mpya ambayo
imeigharimu serikali Dola za Kimarekani Milioni 1.7 ambapo ni zaidi ya
Milioni 400 za kitanzania kutawapa wao motisha ya kufanya kazi kwa
kutumia kifaa cha kisasa na chenye kufanya kazi kwa haraka.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akitoka katika ofisi ya Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali hiyo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto).
Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni
daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) pamoja
na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari
bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
Dkt. Juma Mfinanga (kulia) kuelekea kwenye chumba cha vipimo vya CT Scan
pamoja na MRI alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari
4, 2016.
Baadhi
ya watumishi katika kitengo cha vipimo cha MRI wakiandaa kitanda kwa
ajili ya kumpokea mgonjwa wa kipimo cha MRI (hayupo pichani) kama
walivyokutwa na mpiga picha wa wetu.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata taarifa ya idadi ya wagonjwa
waliofanyiwa vipimo tangu mashine hiyo ipone kutoka kwa Mkuu wa Idara ya
Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare
(kulia).
Mkuu
wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora
Rwakatare akizungumza jambo na waandishi wa habari katika chumba cha
vipimo vya MRI wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Naibu Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.
Dk. Hamisi Kingwangalla, Januari 4, 2016.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya chumba cha vipimo vya MRI
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam
alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan
iliyonunuliwa hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru
(kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa
na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na
muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona
mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho
wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya
ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa
kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya
Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa kwenye dirisha la malipo ya matibabu
hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya, Januari 4,
2016.
Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa
wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma
Mfinanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla
aliyetembelea kitengo chake, Januari 4, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akiendelea kupewa maelezo ya namna wananchi
wanavyohudumiwa katika kitengo hicho na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa
wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma
Mfinangaakitoa maelezo ya ubao maalum unaowaongoza madaktari na
wagonjwa wanaohudumiwa katika kitengo hicho kwa Naibu Waziri wa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi
Kingwangalla.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akikagua wodi mpya ya wagonjwa mahututi
(ICU) ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence
Mseru akimtembeza Mh. Naibu Waziri kwenye wodi hiyo.
Post a Comment