PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAHITIMU WAMETAKIWA KUONDOKANA NA DHANA YA KUAJIRIWA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuondokana na dhana ya kuajiriwa na   badala yake wawe wabunifu...

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuondokana na dhana ya kuajiriwa na  badala yake wawe wabunifu na kutengeneza ajira  zitakazosaidia kupunguza tatizo sugu linalowakabili wahitimu wengi.

Hayo yameelezwa na Dokta  Godwin Lekundayo ambaye ni Askofu wa kanisa la Waadventista Wasabato kanda ya kaskazini mwa Tanzania alipokua akihutubia katika mahafali ya tisa ya chuo kikuu cha Arusha  yaliyofanyika  chuoni hapo,Askofu huyo alisema kuwa kutokana na ugumu ulioko kwenye soko la ajira wahitimu hawana budi kufikiria kujiajiri.

Askofu Godwin  alisema kuwa kutokana na ufinyu wa nafasi za ajira serikalini na sekta binafsi  wasomi  wanapaswa kuamka na kufikiria kujiajiri zaidi kuliko kuajiriwa .

``najua kujiajiri kunahitaji mitaji, ila ni vyema kufanya hivyo ili kurahisisha maisha yetu, ya jamii, na kuondokana na mawazo ya kuajiriwa tu, kwa kuwa soko la ajira ni gumu kwa sasa.`` alisema askofu huyo.

Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa, Emmanuel Matiku aliwataka wahitimu kutumia elimu zao vizuri kwa kuwasaidia wazazi waliowasomesha ili kuwakwamua katika umasikini kwa kuwa wamejifunga mkanda kuhakikisha wanao wanasoma na kuhitimu masomo yao.

``elimu  mliyopata msiitumie kwa faida zenu binafsi, zitumieni kuwakwamua wazazi katika umasikini, na kuielimisha jamii yote`` Alisema Makamu huyo

Kiongozi wa wanafunzi waliohitimu  Bw Jackson Elias kwa niaba ya wanafunzi wengine aliusihi uongozi wa chuo kikuu cha Arusha kuendelea kutatua kwa wakati changamoto wanachuo ikiwemo suala la mikopo ili kuwawezesha wanachuo waliopo kusoma kwa furaha kama walivyosoma wao.

Zaidi ya wahitimu 1,000 walihitimu katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahada kwenye fani mbalimbali ikiwemo elimu, biashara na lugha.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top