NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Wadau na Mashabiki wasoka jijini Arusha
waeelezwa kusikitishwa na mwenendo wa timu yao ya AFC kutokana na
kupoteza michezo yake yote mitatu tangu msimu wa ligi daraja la pili uanze.
Mwishoni mwa timu ya AFC ililala kwa
bao 1-0 dhidi ya JKT Rwankoma mchezo uliopigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid,
huku mashabiki walioshuhudia mpambano huo wakiwa na huzuni kubwa kutokana na
kiwango kibovu kilichoonyeshwa.
Wakizungumza mara baada ya mpambano huo
kumalizika ,Mmoja wa mashabiki hao Edwini Myuka alieleza kuwa
mwenendo mbovu wa timu ya AFC kwanza unasababishwa na wachezaji wenyewe
kutoonyesha ushirikiano kwani wamekuwa wakipata nasafi na kushindwa kuzitumia
ipasavyo.
“Kweli soka la Arusha limeendelea kuwa
chini pia likisababishwa na uongozi wa chama cha mpira mkoani hapa
kushindwa kutoa ushirikiano kwa timu hii ya wakazi wa jiji la Arusha pasipo
kuwaonyesha ushirikiano wa aina yeyeote kwani timu imekuwa ikijiendea yenyewe
tu ikionekana kukata tamaa.”alieleza Myuka.
Shabiki mwingine Ally Mohamed Ally
alisema kiwango cha timu cha AFC kimeshuka sana ukilinganisha hapo
awali Kutokana na wadau mbalimbali wa soka kushindwa kabisa kuiunga mkono,Kinachotakiwa
timu ikae chini iweze kujipanga upya msimu ujao.
Omary Habiby aliweza kuiandikia timu
yake ya JKT Rwamkomna bao moja na la pekee lililodumu kwa dakika 90 za
mchezo baada ya kuachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja nyavuni.
Kocha wa timu ya
JKT Rwamkoma Said Ally Mbwana alisema kuwa Nidhamu ya mchezo
imeisaidia timu yake kuweza kuibuka na ushindi wa kwanza tena ugenini
kutokana na wachezaji kuonyesha kujituma zaidi tangu mpira ulipoanza.
Hata hivyo timu ya AFC Imepoteza
michezo yake mitatu iliyocheza tangu kuanza kwa ligi ikiwemo michezo yake
iliyocheza na timu ya Pamba ya jijini Mwanza na kufungwa mabo 2-0 ,vile vile
ilifungwa na timu ya Alliance Spors Academy pia ya Mwanza mbao 3-0 .
Post a Comment