PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MADINI FC WAWAPIGA MKWARA WAJESHI WA OLJORO JKT.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya Madini Fc inayoshiriki Ligi daraja la Pili (SDL) imeanza tambo dhidi ya JKT Oljro inayoshiriki L...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya Madini Fc inayoshiriki Ligi daraja la Pili (SDL) imeanza tambo dhidi ya JKT Oljro inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza (FDL), kuelekea Katika mchezo wa Kombe la shirikisho (FA) Utakaochezwa leo jumatano katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Madini Fc imeshida michezo miwili kati ya Mitatu tangu kuanza kwa ligi daraja La Pili, ilipoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Alliance kwa kufungwa ugenini mabao 2-0, kisha kushinda michezo miwili iliyofuata,waliifunga JKT Rwankoma Bao 1-0 kisha kuisambaratisha Pamba mabao 2-0.  

Madini Fc Wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo mra baada ya kuifungashia vilago timu ya AFC kwa kuifunga mabao 2-0.

Mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Klabu hiyo Madaraka Bendera, alisema kuwa wanauhakika wa kushinda mchezo huo kutokana na ubora wa kikosi chake.

“hatuwezi kuiogopa Oljoro kwa kuwa wanashiriki Ligi daraja la kwanza na sisi tupo ligi daraja la Pili, wasahau hilo, ni utofauti tu wa ligi lakini tupo vizuri ziadi ya Wao, na yeyote anayecheza vizuri basi ndiye mwenye nafasi kubwa ya Kushinda Mchezo” alisema Bendera.  

Aliongeza kuwa timu zinapocheza katika michuano hiyo zinakuwa na tahadhri kubwa kutokana na kanuni za michuano hivyo ilivyo ambapo katika kila mchezo mmoja lazima atoke.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top