PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JKT OLJORO YAANZA KUANIKA KIKOSI KIPYA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya JKT Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza (FDL) imeaanza kuanika baadhi ya wachezaji walioin...

NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya JKT Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza (FDL) imeaanza kuanika baadhi ya wachezaji walioingia katika dirisha dogo la ushajiri, litakalofungwa wiki hii.

JKT Oljoro inaongoza katika kundi lao ikiwa na Pointi 14  baada ya kushuka dimbani mara saba, na kufanikiwa kushinda michezo minne sare michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja dhidi ya dhidi ya Panone Fc bao 4-0. Katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa katika uwanja wa ushirika Moshi.

Katibu mkuu wa Klabu hiyo Hssein Nalinga alisema kuwa, kuna wachezaji wengi kutoka timu kubwa wamefika kufanya zoezi ili wapate kusajiliwa katika usajili wa dirisha dogo, ambapo Oljoro wananafasi sita za kuziba mapengo waliyonayo.

“Hatuwezi kumzuia mchezaji kuja kufanya mazoezi na timu yetu, wamefika wachezaji Kutoka Simba, Mtibwa, Geita Gold Star na Polis Morogoro lakini tumemwachia Kocha afanye kazi yake ili mwisho wa siku yeye ndiye atajua nani anafaa”.

“Tulikuwa na Mapungufu katika nafasi ya walinzi,washambuliaji, na Kiungo, ambapo tulikuwa na wachezaji wachache katika nafasi hizo hivyo akiumia mchezaji inakuwa vigumu kumpata wa kuziba nafasi kwa haraka” alisema Nlinga.

Tayari Oljoro wamefanikiwa Kumrudisha msambuliaji wao wa zamani Sino Agustino ambaye alitimukia katika klabu ya Geita Gold star na sasa amerejea kuongeza nguvu katika nafasi ya ushambuliaji ya Timu hiyo.

Nalinga aliongeza kuwa Oljoro ni timu yenye uzoefu mkubwa kuanzia ligi kuu hadi ligi daraja la kwanza, hivyo watacheza kwa tahadhari kubwa ili kuendelea kubaki kileleni na hatimaye kurudi ligi kuu msimu ujao.

Mchezo wa kwanza katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo utakaoanza Disemba 26, JKT Oljoro Wataikaribisha Panone Fc katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top