PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: FUTURE STARS YATWAA NDOO LA CHIPUKIZI CUP.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA Timu kutoka taasisi ya kuinua na kukuza vipaji kwa vijana Future stars Academy imefanikiwa kutwaa ubingwa...

NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA

Timu kutoka taasisi ya kuinua na kukuza vipaji kwa vijana Future stars Academy imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa vijana walio na umri wa miaka 18  baada ya kuisambaratisha timu ya Arusha Region Soccer kwa Bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa TGT jijini hapa.

Kwa wenye umri wa miaka 16, kwa mara ya kwanza kushiriki michuano ya kombe la Chipukizi, Timu  ya Ruaha football Academy kutoka Mkoani Iringa ilitwaa ubingwa kwa vijana wa umri huo baada ya kumaliza mashindano ikiwa na jumla ya pointi 7 nyuma ya Wenyeji wao Timu ya Future stars academy iliyomaliza kwa pointi 5.

Katika umri wa miaka 14 timu ya Soca Ndogo ilitwaa ubingwa na kufuatiwa na timu ya future stars.

Timu kutoka nchini Kenya zimefanikiwakuonyesha ushindani wa kipekee baada  kutetea ubingwa wa mashindano ya vijana ya  nchi za Afrika Mashariki baada ya kuibuka na ushindi kwa mara nyingine kwa umri wa miaka 10 na 12.

Lingi Ndogo Academy kutoka Kenya ni timu ambayo ilitetea taji lake baada ya kuibuka na ushindi mnono katika mchezo wa fainali  Kwa jumla ya magoli  3-0 dhidi ya timu ya All Saints Cathedral nayo  kutoka nchini  Kenya huku kwa umri wa miaka 12  Ligi Ndogo academy walitetea taji lao katika umri huo baada ya kusambaratisha timu ya majirani wenzao Express Soccer kwa magoli 4-0.

“Pamoja na timu nyingi kutoka nchini Kenya pia timu za hapa nchini zimeweza kufanya vizuri,kumekuwa na ushindani mkubwa tofauti na mashindano yaliyopita vile vile  wageni wetu wameridhishwa na viwanja tulivyoendesha michuano kwa kusema kuwa vipo katika hali nzuri ya kimichezo.”alisema Alfred Itaeli ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya Future stars.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top