NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu
ya Madini Fc inayoshiriki Ligi daraja la Pili (SDL) imeanza tambo dhidi ya JKT
Oljro inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza (FDL), kuelekea Katika mchezo wa Kombe
la shirikisho (FA) Utakaochezwa leo
jumatano katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Madini
Fc imeshida michezo miwili kati ya Mitatu tangu kuanza kwa ligi daraja La Pili,
ilipoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Alliance kwa kufungwa ugenini mabao 2-0, kisha
kushinda michezo miwili iliyofuata,waliifunga JKT Rwankoma Bao 1-0 kisha kuisambaratisha
Pamba mabao 2-0.
Madini
Fc Wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo mra baada ya kuifungashia
vilago timu ya AFC kwa kuifunga mabao 2-0.
Mjumbe wa
Kamati ya Ufundi wa Klabu hiyo Madaraka Bendera, alisema kuwa wanauhakika wa
kushinda mchezo huo kutokana na ubora wa kikosi chake.
“hatuwezi
kuiogopa Oljoro kwa kuwa wanashiriki Ligi daraja la kwanza na sisi tupo ligi daraja
la Pili, wasahau hilo, ni utofauti tu wa ligi lakini tupo vizuri ziadi ya Wao,
na yeyote anayecheza vizuri basi ndiye mwenye nafasi kubwa ya Kushinda Mchezo”
alisema Bendera.
Aliongeza
kuwa timu zinapocheza katika michuano hiyo zinakuwa na tahadhri kubwa kutokana
na kanuni za michuano hivyo ilivyo ambapo katika kila mchezo mmoja lazima
atoke.
Post a Comment