NA;
YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu ya JKT Oljoro
inayoshiriki ligi daraja la kwanza (FDL) imeaanza kuanika baadhi ya wachezaji
walioingia katika dirisha dogo la ushajiri, litakalofungwa wiki hii.
JKT Oljoro inaongoza
katika kundi lao ikiwa na Pointi 14 baada ya kushuka dimbani mara saba,
na kufanikiwa kushinda michezo minne sare michezo miwili na kufungwa mchezo
mmoja dhidi ya dhidi ya Panone Fc bao 4-0. Katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa
katika uwanja wa ushirika Moshi.
Katibu mkuu wa
Klabu hiyo Hssein Nalinga alisema kuwa, kuna wachezaji wengi kutoka timu kubwa
wamefika kufanya zoezi ili wapate kusajiliwa katika usajili wa dirisha dogo,
ambapo Oljoro wananafasi sita za kuziba mapengo waliyonayo.
“Hatuwezi kumzuia
mchezaji kuja kufanya mazoezi na timu yetu, wamefika wachezaji Kutoka Simba,
Mtibwa, Geita Gold Star na Polis Morogoro lakini tumemwachia Kocha afanye kazi
yake ili mwisho wa siku yeye ndiye atajua nani anafaa”.
“Tulikuwa na
Mapungufu katika nafasi ya walinzi,washambuliaji, na Kiungo, ambapo tulikuwa na
wachezaji wachache katika nafasi hizo hivyo akiumia mchezaji inakuwa vigumu
kumpata wa kuziba nafasi kwa haraka” alisema Nlinga.
Tayari Oljoro
wamefanikiwa Kumrudisha msambuliaji wao wa zamani Sino Agustino ambaye
alitimukia katika klabu ya Geita Gold star na sasa amerejea kuongeza nguvu
katika nafasi ya ushambuliaji ya Timu hiyo.
Nalinga aliongeza
kuwa Oljoro ni timu yenye uzoefu mkubwa kuanzia ligi kuu hadi ligi daraja la
kwanza, hivyo watacheza kwa tahadhari kubwa ili kuendelea kubaki kileleni na
hatimaye kurudi ligi kuu msimu ujao.
Mchezo wa kwanza
katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo utakaoanza Disemba 26, JKT Oljoro
Wataikaribisha Panone Fc katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Post a Comment