NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA
Timu kutoka taasisi ya kuinua na kukuza vipaji kwa vijana Future
stars Academy imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa vijana walio na umri wa miaka
18 baada ya kuisambaratisha timu ya Arusha Region Soccer kwa Bao 1-0
katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa TGT jijini hapa.
Kwa wenye umri wa miaka 16, kwa mara ya kwanza kushiriki michuano
ya kombe la Chipukizi, Timu ya Ruaha football Academy kutoka Mkoani
Iringa ilitwaa ubingwa kwa vijana wa umri huo baada ya kumaliza mashindano
ikiwa na jumla ya pointi 7 nyuma ya Wenyeji wao Timu ya Future stars academy
iliyomaliza kwa pointi 5.
Katika umri wa miaka 14 timu ya Soca Ndogo ilitwaa ubingwa na
kufuatiwa na timu ya future stars.
Timu kutoka nchini Kenya zimefanikiwakuonyesha ushindani wa
kipekee baada kutetea ubingwa wa mashindano ya vijana ya nchi za Afrika
Mashariki baada ya kuibuka na ushindi kwa mara nyingine kwa umri wa miaka 10 na
12.
Lingi Ndogo Academy kutoka Kenya ni timu ambayo ilitetea taji lake
baada ya kuibuka na ushindi mnono katika mchezo wa fainali Kwa jumla ya
magoli 3-0 dhidi ya timu ya All Saints Cathedral nayo kutoka
nchini Kenya huku kwa umri wa miaka 12 Ligi Ndogo academy walitetea
taji lao katika umri huo baada ya kusambaratisha timu ya majirani wenzao
Express Soccer kwa magoli 4-0.
“Pamoja na timu nyingi kutoka nchini Kenya pia timu za hapa nchini
zimeweza kufanya vizuri,kumekuwa na ushindani mkubwa tofauti na mashindano
yaliyopita vile vile wageni wetu wameridhishwa na viwanja tulivyoendesha
michuano kwa kusema kuwa vipo katika hali nzuri ya kimichezo.”alisema Alfred
Itaeli ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya Future stars.
Post a Comment