PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: LIGI MKOA WA KILIMANJARO YAFIKIA PATAMU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro inatarajia kuendelea tena leo jumatatu kwa michezo kadhaa ...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA
Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro inatarajia kuendelea tena leo jumatatu kwa michezo kadhaa Kuchezwa ili kusaka nafasi ya kuingia sita bora ya ligi hiyo.

Timu ya Mvuleni itachez na Lang’ata katika uwanja wa Magereza, Kilimanjaro Fc wataikaribisha Machame United katika uwanja wa Jamuhuri, wakati katika uwanja wa Ushirika timu ya Kitoyosa watacheza na Ushirika Fc.

Ligi hiyo inajumuisha timu kutoka wilaya na Manispaa zote zilizokuwa ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwemo Wilaya ya Hai, Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Siha,Vunjo na Rombo

Katibu Mkuu wa chama cha Soka Mkoani humo Mohamed Musa, alisema ligi hiyo inajumla ya timu 18 ambazo zigawanywa makundi mawili, huku kila kundi likiwa linatimu tisa.

Katika kundi la kwanza kuna timu ya Afro Boys, Kilimanjaro Fc, Reli Manispaa, Ushirika United, Kitayosa FC, Machame United,nyingine ni pamoja na KIA Sc, Machava na Sango Fc.

Kundi B limebeba timu ya Lang’ata, Hai, Forest Fc, Mvulen , New generation, Pozolana, Upendo FC, Soweto united na Kilimanjaro Rangers.

Kila kundi litatoa timu tatu ambazo zitaingia hatua ya Sita bora itakayoaanza januari 3 mwaka ujao ili kumpata Bingwa Wa Mkoa Atakayewakilisha Mkoa huo kwenye ligi ya Mabingwa wa Mikoa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top