Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (44) amekana kumtukana Mkuu wa wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda tarehe 14 Desemba 2015 walipokutana katika
Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd. kilichopo eneo la External Mabibo
kwa madhumuni ya kutatua mgogoro kati ya wafanyakazi na uongozi wa
kiwanda hicho
Katika kesi inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu,
Wakili wa Serikali mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alimsomea mshtakiwa
maelezo ya kesi hiyo ambapo baadhi ya mashtakiwa aliyakana.
Akisomewa maelezo ya kesi, Saed Kubenea alikiri kuwa ni mbunge wa Ubungo
na pia alikiri kuwa anamfahamu mlalamikaji katika kesi hiyo kuwa ni
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda na kwamba ni kweli kuwa tarehe 14
Desemba 2015 alifika katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd
kulikokuwa na mgomo wa wafanyakazi.
Hata hivyo, alipoelezwa kuwa anashtakiwa kwa kosa la kumtolea lugha
chafu Makonda ambapo alimwita kuwa ni kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo
chake ni cha kupewa kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa
amani na utulivu; Saed Kubenea alikana.
Kufuatia Kubenea kukana mashitaka yanayomkabili, Hakimu mkazi mkuu wa
mahakama hiyo , Thomas Simba alisema mashahidi sita wa upande wa
mashtaka wataanza kutoa ushahidi wao Januari 20 na 21, 2016 katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Post a Comment