Home
»
UCHAGUZI MKUU 2015
» Lipumba Amtwika Zigo Dr Shein Mgogoro Zanzibar....Asema Mgogoro Utakwisha Iwapo Dr Shein Atakubali ZEC Iendelee Kutangaza Matokeo
Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kumaliza
mgogoro wa Zanzibar.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mgogoro wa
Zanzibar utamalizwa kwa Dk Shein kuiruhusu Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar
(ZEC) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.
Alisema pamoja na mazungumzo yanayoendelea kati ya CUF na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Shein ndiye mwenye uwezo kuumaliza mgogoro
huo.
“Mazungumzo yanaendelea na hatujui yatafika mwisho lini, lakini Dk
Shein ndiye anayeweza kuifanya Zanzibar iwe na amani au vurugu,
ninashauri aruhusu kutangazwa kwa matokeo,” alisema.
Alisema amani na utulivu uliopo Zanzibar wakati wananchi wakisubiri
hatima ya mgogoro huo, haiwezi kuwa ya kudumu kwani ikiamuliwa uchaguzi
urudiwe wapo ambao hawatakubali.
Profesa Lipumba alisema uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa huru na haki na
hata watazamaji wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali walishangaa matokeo
yake kufutwa.
Alisema wananchi wa Zanzibar walishapiga kura na kwamba wanachosubiri ni
matokeo vinginevyo haki yao ya kidemokrasia itakuwa imechezewa.
Oktoba 28 mwaka huu, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta
uchaguzi huo kwa kile alichosema kulikuwa na kasoro ndani ya tume
yenyewe na kwenye vituo vya kupigia kura.
Profesa Lipumba alisema mgogoro huo ukiendelea, utakwamisha msaada wa
Dola za Marekani 472.8 milioni uliokuwa utolewe na Shirika la Maendeleo
ya Milenia (MCC) la Marekani.
Alisema Bodi ya MCC ilikutana Desemba 16 na kushindwa kupitisha msaada
huo kwa Tanzania huku hoja kubwa ikiwa kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi
Mkuu Zanzibar.
Alisema miongoni mwa matumizi ya msaada huo ilikuwa kuunganisha wateja wapya 300,000 kupata umeme.
“Hapa tunategemea busara za Dk Shein kuumaliza mgogoro ili tupate
msaada huo wenye masilahi ya Taifa au kuendelea na mgogoro na kuukosa
msaada huo,” alisema.
Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena
Sakaya alisema huu ni muda mwafaka kwa Dk Shein kuweka masilahi ya
Wazanzibari mbele.
Alisema atawekwa kwenye vitabu vya historia kama atafanya uamuzi wa
kuruhusu kutangazwa kwa matokeo hata kama viongozi wenzake wa CCM
hawatapenda uamuzi huo.
About Author

Advertisement

Related Posts
- JENGO LA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO KUWA KIVUTIO CHA KIHISTORIA CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA UTALII JIJINI ARUSHA10 Apr 20180
Na Hamza Temba - WMU........................................................JENGO la kit...Read more »
- Maalim Seif Amjia Juu Msajili Sakata la Kufukuzwa Uanachama Wanachama Saba wa CUF19 Aug 20170
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amemjibu Msajili wa...Read more »
- Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imewateua 8 kuwa Wabunge wa Viti Maalum CUF27 Jul 20170
Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzan...Read more »
- Baada ya Jecha Kudai Alikuwa Sahii Kufuta Uchaguzi ZNZ,Maalim Seif Aibuka na Haya..!!!24 Jan 20170
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema ameshamalizana na mwenyekiti wa Tume y...Read more »
- Sumaye - Sishtushwi na Utendaji Kazi wa Magufuli Kwani Anatekeleza Ilani ya Chadema16 Jan 20170
WAKATI Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli akitekeleza masuala...Read more »
- Kikwete Atoa Dongo "Wapo Watu Walidhani CCM ingekufa na Walishajiandaa na Salamu za Rambirambi"22 Jul 20160
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais mstaafu Jakaya Kikwete, a...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.