RAIS Paul Kagame wa Rwanda
amefurahishwa na hatua ambazo Rais John Magufuli anazichukua, hasa
katika usimamizi na utendaji kazi wa bandari huku akimhakikishia kuwa
Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania, hasa katika kuitumia Bandari
ya Dar es Salaam.
Siku chache baada ya kuingia
madarakani, Rais Magufuli akimtumia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
alifanya ziara ya ghafla katika Bandari ya Dar es Salaam, ambako
alifichua ufisadi wa mabilioni ya shilingi kutokana na upotevu wa
makontena, ambayuo hayakulipiwa kodi stahili kwa serikali.
Kutokana na ufisadi huo, Rais
aliivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA),
alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadhi Massawe na
kusimamisha maofisa kadhaa wa bandari hiyo na wengine wanaohusika na
usimamizi wa bandari kavu.
Aidha, alimsimamisha kazi Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade na maofisa wengine
wa mamlaka hiyo, ambao miongoni mwao tayari wamepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutokana na
ubadhirifu huo.
Kutokana na hilo, Rais Kagame kupitia
kwa Balozi wake nchini, Uegene Kayihura, amempongeza Rais Magufuli kwa
hatua alizochukua kusafisha uozo katika bandari hiyo, ambayo Rwanda
inapitisha asilimia 70 ya mizigo yake. Dk Magufuli jana alikutana na
kufanya mazungumzo na Balozi Kayihura Ikulu jijini Dar es Salaam.
Post a Comment