PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI PICHA ZA ZIARA YA NAIBU WAZIRI MHE. POSSI KATIKA KITUO CHA WAZEE NUNGWI KIGAMBONI JIJINI DARESALAAM
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Naibu Waziri (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni alipotembelea Kituo cha kulea watu we...
Naibu Waziri (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni alipotembelea Kituo cha kulea watu wenye ulemavu cha Nunge Kigamboni Dar es Salaam hivi karibuni, pembeni ni Afisa Mfawidhi Makazi ya Wazee Bw. Ojuku Mgesi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Afisa Mfawidhi Makazi ya Wazee wa kituo cha kulea watu wenye ulemavu cha Nunge Kigamboni, Bw. Ojuku Mgesi akimuonesha Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) banda linalotumiwa kufuga kuku ikiwa ni sehemu ya mradi wa wazee wa kituo hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (mwenye miwani) akimsikiliza Bw. Salum Omari mwenye ugojwa wa ukoma alipokuwa akielezea changamoto za uvamizi wa ardhi katika Kituo cha Kulea watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge Kigamboni. Tarehe 28, Desemba, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akieleza jambo kwa mmoja wa wakazi wa Kituo cha Watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge juu ya umuhimu wa kuhama na kuwapisha watu wenye matatizo wenye ulemavu.


Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Bi. Consolata Edward alipokuwa akieleza changamoto anazokumbana nazo juu ya tatizo la Kifafa kinachomfanya wakati mwingi kupoteza fahamu na kushindwa kufanya mambo yake kwa ufasaha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top