NA;
YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
MAAFANDE Wa timu ya JKT
Oljoro ya jijini Arusha Mwishoni mwa wiki wameendelea kugawa dozi kwa timu
pinzani baada ya kufanikiwa kuwalaza timu ya Geita Gold Sports ya mkoani Geita
kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa ndani ya
dimba la sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Baada
ya Ushindi huo timu hiyo ya Oljoro imefikisha jumla ya pointi 11 na kushika
usukani wa kundi hilo sawa na wapinzani wao Geita Gold Sport huku
zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Swalehe
Hussein aliweza kuiandikia timu yake ya Jkt Oljoro Bao la kuongoza dakika
ya 17 kwa njia ya kichwa ,
baada ya kupokea mpira wa kurushwa kutoka kwa Yusuph Machogote,
Bao lilidumu kipindi chote cha dakka 45 za kipindi cha kwanza.
JKT Oljoro
waliingia kipindi cha pili wakiwa na malengo ya kufunga mabao
zaidi,huku ikiwachukua dakika moja tangu watoke mapumziko kuandika bao la pili
lililofungwa na Lucas Charles dakika ya
46 na timu ya Geita Gold Sports ilijipatia bao lake la kufutia
machozi lililowekwa nyavuni na mchezaji Hillary Bingwa.
Akizungumza
mara baada ya pambano hilo kocha msaidizi wa timu ya JKT Oljoro Joely
Mwambegele alisema kuwa timu yao itahakikisha inamaliza raundi hii ya kwanza
ikiwa inaongoza kundi hilo kwani wanataka waweze
kushiriki ligi kuu msimu ujao ambapo aliwaomba wakazi wa Arusha kuendelea
kuwaunga mkono zaidi.
Kwa
upande wake kocha msaidizi wa timu ya Geita Gold Sports , Teru Yusuph alieleza
kuwa mchezo ulikuwa mzuri na timu yake imeweza
kucheza mpira vyema.
“Bahati
ya kuibuka na ushindi haikuwa ya kwao na tutajipanga zaidi kwa michezo ijayo kwa
ligi bado inaendele na tuna nafasi ya kulejesha matumaini yetu kwa wapenzi wetu”
alisema Yusuph.
Mchezo
mwingine wa ligi daraja la kwanza ulichezwa katika uwanja wa Ushirika Mjini
Moshi ,Mkoani Kilimanjaro ambapo ulimalizika kwa wenyeji Timu ya Panone
Fc kuibuka kidedea kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 ,Dhidi ya timu ya
Polisi Mara.
Timu
ya JKT Oljoro itashuka tena uwanjani jumamosi ijayo ambapo
itawakaribisha maafande wenzao wa Timu ya Polisi Tabora huku timu ya Panone FC ya
Mkoani Kilimanjaro itakuwa ikicheza katika uwanja wao wa nyumbani na timu ya
Rhino Rangers ya mjini Tabora.
Post a Comment