NA; YOHANA CHALLE
ARUSHA.
Timu ya AFC
ya jijini hapa ambayo inajiandaa na kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya
Taifa (SDL), Imeongeza kocha na wachezaji wapya ili kuimalisha zaidi kikosi
hicho ambacho ni kipenzi kikubwa cha wakazi wa Arusha.
Akizungumzia hilo katibu msaidizi wa
timu ya AFC, Charles Mwaimu alisema kuwa tayari wameongeza wachezaji watatu ambao
ni Athuman Ponda, Abdallah Kidula na Amour Hamad.
Huku Kocha
atakayekinoa kikosi hicho ni Mussa Rashid Omari aliyekuwa kocha wa timu ya
Bishop Durning.
“Hatuhitaji
lawama kwa sasa tumefanikiwa kumpata kocha mahili ambaye ni Mkazi wa Arusha na
Mpenzi wa AFC na wachezaji watatu, mmoja kutoka Tanga, mwingine Dar es Salaam
na wa tatu kutoka Zanzibar” aliesma Mwaimu.
Aliongeza kuwa
Athuman Ponda alikuwa mchezaji wa Coastal Union Miaka ya nyuma ila kwa sasa
alikuwa anafanya mazoezi na timu ya Villa Squad ya Dar es Salaam baada ya
kukosa timu kwa muda mrefu.
Alisema kuwa
wachezaji wote wameshaingia kambini mpaka hivi sasa na hakuna majeruhi, isipokuwa Martin Teobard aliyepata matatizo
ya kifamilia hivyo yupo kwao Mkoani Morogoro na ifikapo jumatatu atakua amesharudi kambini kuendelea
na mazoezi.
Hadi sasa
kikosi cha AFC kinafanya mazoezi na marafiki zao wakubwa kikosi cha JKT Oljoro
inayoshiriki Ligi daraja la kwanza hivyo hiyo ni faida kubwa kwa timu ya AFC
kujua mapungufu yao kabla ya SDL kuanza.
Post a Comment