NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Kocha Mkuu
wa JKT Oljoro Ally Mohamedi amesema kuwa watahakikisha wanabadili kikosi cha
timu hiyo pindi dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Septemba 15.
Kocha huyo
alisema haya mwishoni mwa wiki baada ya mchezo Katika mwendelezo wa Ligi daraja
la kwanza (FDL) dhidi ya Poloisi Tabora jijini hapa ambapo katika mchezo huo
Oljoro walishinda bao 1-0.
Mchezo huo ulikuwa
wa kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa ligi daraja la Kwanza (FDL), ulichezwa
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini hapa, na kushuhudiwa na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura.
Oljoro
imefanikiwa kubaki kileleni ikijikusanyia alama 14 na kuiacha Polisi Tabora
ikiwa na alama 11 timu ambayo ilikuwa inakimbizana na Oljoro Kileleni.
katika
mchezo huo Polisi walionekana kuwamudu wenyeji wao kwa kipindi chote cha dakika
45 za kipindi cha kwanza kabla ya Swalehe Iddi kwafungia Oljoro Bao pekee na la
ushindi mnamo dakika ya 61 baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Paulo
Malipesa.
Kocha Mkuu wa Oljoro Ally Mohamedi maarufu kama Babu
Kidi alizungumza kwa mara ya kwa mna waandishi wa habari tangu atue kwenye timu
hiyo na kusema kuwa mara baada ya kumalizika mzunguko huo kilichobaki ni
kukiimalisha zaidi kikosi chake.
"Nimefurahishwa
wachezaji wangu wamebadilika na wanajitua kwa kuwa wameshafahamu kuwa wanahitaji
kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao hivyo kila mchezaji acheza kwa lengo
moja tu tulilojiwekea la kupanda ligi kuu" alisea Mohamedi
Aliongeza
kuwa watahakikisha wanaongeza nguvu pindi dirisha Dogo la usajili litakapo
funguliwa Septemba 15 na kufanya timu inabaki kileleni hadi mwisho wa FDL.
Post a Comment