Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wananchi wa
Kijiji cha Nayobi kilichopo tarafa ya
Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamelalamikia kero ya uhaba wa
maji inayowasababishia kukesha kwenye bomba la kijiji kwa takribani siku tatu
wakisubiri maji jambo linalopelekea shughuli za kijamii na kiuchumi kusimama
kwa muda mrefu na kinamama kutembea umbali mrefu wakitafuta huduma hiyo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa kwa muda mrefu wamekua
wakiteseka kupata huduma za maji huku kinamama wajawazito wakijifungulia
bombani apo baada ya kukaa kwa muda wakitafuta maji huku wengine wakilazimika
kukesha na watoto wadogo .
Wanakijiji
Daniel Sereki na Rehema Laizer
na wamesema kuwa kwa sasa wanakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa maji
pamoja na chakula na hata pale wanapopata chakula hukosa maji ya kupikia
chakula hicho na kuziacha familia zao zikitaabika kwa njaa.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kijiji Naiyobi Meleji Sikoni amesema kuwa kwa muda wa miaka 20
wamekua wakikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji hivyo ameiomba serikali na
mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
iwasaidie kutatua tatizo hilo sugu linalowaathiri wananchi wengi.
Mgombea
Ubunge Jimbo la Ngorongoro Wiliam Olenasha
ameeeleza kisikitishwa na wananchi wanaoteseka kwa kero ya maji ambayo
hushirikiana na mifugo katika matumizi yake hivyo ameaidi kutatua kero hiyo
pindi atakapopata ridhaa ya kuongoza wilaya hiyo.
Wilaya ya
Ngorongoro inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji pamoja na chakula hasa
katika kipindi hiki cha kiangazi ,juhudi zinahitajika kwa upande wa serikali na
Mamlaka ya Ngorongoro ili kuweza kuwanusuru wananchi na baa la njaa pamoja na
uhaba wa maji.
Post a Comment