Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
RAIS
DK.Jakaya Kikwete ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kufanya
tathimini upya kwa wakazi wa vijiji vitatu wanaopisha bandari ya
Bagamoyo.
Dk.Kikwete
ameyasema hayo leo Bagamoyo wakati wa kuweka jiwe la msingi la
uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ,amesema kuwa wananchi
wasiondoke katika maeneo yao wakiwa na manunguniko.
Amesema
kuwa mradi wa ujenzi ni mkubwa hivyo wananchi wanatakiwa kupewa haki
yake kutokana na eneo ikiwa pamoja na kujengewa nyumba katika kuanza
upya kwa makazi ya Kidagoni.
Rais
Kikwete amesema mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo umekuja wakati
mwafaka kwa kuongeza fursa nyingi baada ya kukamilika kwa mradi huo na
kuongeza uchumi wa nchi.
Aidha
ameiagiza Mthamini wa Halmashauri kutafutiwa sehemu nyingine kutokana
na kufanya tathimini isiyoendana na malipo hali ya wakazi hao ambao
wameachia eneo hilo kwa ajili ya uchumi.
“Nchi
haiwezi kuwa safi kuwepo mradi mkubwa wa bandari kubwa Afrika lakini
wananchi waliocha eneo hilo wakiwa wananungunika kwa kupuchwa mali zao
kwa ajili ya mtu mmoja tu”amesema Rais Jakaya.
Rais
Dk.Jakaya Kikwete akizungumza leo wananchi wa Bagamoyo katika hafla
ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Rais Dk.Jakaya Kikwete akifungua pazia kwa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo leo.
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza leo wananchi wa Bagamoyo katika hafla
ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza leo wananchi wa Bagamoyo juu ya ujenzi wa bandari ya Bangamoyo.
Makamu
wa Rais Mtendaji wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China, Dk.Hu Jianhua
akizungumza katika uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo leo.
Sehemu ya viongozi wa waliohudhuria uwekaji wa jiwe la la msingi na uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo leo.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika picha na viongozi mbalimbali baada ya
kuweka jiwe la msingi na ujenzi wa bandari ya bagamoyo leo.
Baadhi ya wananchi wa Bagamoyo waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
( Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya Jamii)
Post a Comment