Mkurugenzi
Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania,
(Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na
salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo hivi karibuni jijini
Mwanza.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MKURUGENZI
Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Amon
Manyama, alisema vita dhidi ya umaskini inakuwa na maana kubwa kama
inalinganishwa na mazingira.
Alisema
kwamba umaskini wa kipato ambao umekuwa ukipiganwa sana kwa sasa
unastahili kupiganwa kwa kuangalia umaskini kutokana na ukweli kuwa
kuboreshwa kwa mazingira ndio hatua kubwa ya kupigana na umaskini katika
sura zote zilizobaki.
Mkurugenzi
msaidizi huyo alisema hayo hivi karibuni mjini Mwanza wakati akielezea
mradi wa mtaji na elimu wa UNDP ambao umefanyiwa kazi kwa pamoja kati ya
shirika hilo, Tume ya Mipango, Hazina na Ofisi ya Makamu wa Rais,
katika mafunzo ya siku moja ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na
Mikopo, yaliyofanyika Mwanza.
Mradi
huo umelenga kuwezesha ushirika wa akiba na mikopo katika wilaya sita
nchini kuwezesha wananchi kushiriki katika kukabili umaskini
unaosababishwa na mazingira.
Akifafanua
alisema kwamba inawezekana muda wa kusubiri kuvuna samaki ziwani
umekwisha kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika ni kupanda samaki ndani au
nje ya ziwa na watu waweze kutumia nafasi hiyo kuboresha maisha yao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi
Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumuni ya mafunzo hayo kwa
washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.
Alisema
hali hiyo pia ipo katika misitu. Wakati watu wanakata misitu unawapa
elimu na mtaji wa kupanda misitu mingine na hivyo mazingira yakaendelea
kubaki na kuwa mtaji wa kukabili umaskini.
Mradi
huo ambao upo katika wilaya sita kwa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka
2021 na ifikapo muda huo utakuwaupo wilaya 21 na kutumika kama kichochea
cha utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu yenye nia ya kupiga
vita umaskini, kuondoa ubaguzi na njaa.
Alisema
mafunzo yaliyotolewa katika kongamano la viongozi mbalimbali wa vyama
vya ushirika vya aina mbalimbali mjini Mwanza kwa msaada wa UNDP na
kutekelezwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii
(ESRF) yamelenga kuwezesha SACCOS kutambua fursa hizo za mazingira
kukabili umaskini.
Alisema
katika mazingira ya sasa wanawake ndio wanaathirika zaidi katika
umaskini kutokana na wao kuwa wazazlishaji na wahudumiaji wa kaya na
kwamba kama kutakuwepo na mabadiliko na mazingira yakatengeneza fursa ya
kupiga vita umasikini wanawake wataendelea kustawi.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na
kijamii (ESRF) ESRF Dk. Tausi Kida alisema lengo la mafunzo hayo ni
kuimarisha ushirika wa akiba na mikopo mkoani Mwanza.
Akizungumzia
historia ya mradi alisema wao kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
(UNEP) pamoja Tume ya mipango, walianza kutekeleza mradi wa kukuza
uchumi, kuleta maendeleo endelevu kupitia utunzaji mazingira, usawa wa
kijinsia na kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia
nchi yaani (PEI) toka mwaka 2014.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na
VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na
Sengerema wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa.
Alisema
tafiti mbili chini ya mradi wa PEI zilizofanyika katika wilaya za
Bunda, Ileje, Sengerema, Bukoba vijijini, Ikungi na Nyasa kubaini
changamoto na fursa zinazopatikana katika wilaya hizo.
Alisema
matokeo ya tafiti yalionyesha umuhimu wa kuzipa uwezo taasisi za
kifedha kama SACCOSS, VICOBA na vikundi mbalimbali vya kifedha kwa
kuzijengea uwezo wa kitaaluma na kifedha.
Alisema
hata hivyo pamoja na matokeo hayo Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) ilitenga na kutoa fungu la fedha na kuipatia benki ya
Twiga ili kukopesha kwa riba nafuu kwenye taasisi kama SACCOSS na VICOBA
kwa lengo kuu kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ili waweze kupata
fursa ya kukuza mitaji yao na kuwafanya muweze kutekeleza fursa hizi
katika maeneo yao.
Post a Comment