Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini
Unguja katika Kijiji cha Mahonda wakati wa ziara fupi ya kukagua miradi
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema Umoja huo utaendelea
kushirikiana na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kukomesha
vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Akizungumza
katika ziara ya kutembelea Dawati la jinsia la Wanawake na Watoto, Mkoa
wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda alisema umoja huo
umelenga kusaidia uwepo wa utawala wa sheria na wenye kujali haki na utu
wa binadamu kupitia mpango mkakati wake uliomo katika malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs) kuanzia mwaka 2016 utakosaidia kuondoa vitendo
hivyo.
Alieleza
kuwa tatizo la udhalilishaji wa kijinsia sio kwa Zanzibar pekee bali
ni la kidunia, hivyo umoja wa mataifa(UN) unawajibu kusaidia juhudi za
serikali kupambana na tatizo hilo.
“Tushirikiane
kwa kila hatua ili kuondosha vitendo hivi kwani ni tatizo na kero kwa
jamii ya Zanzibar pia ni miongoni mwa ishara tosha zinazoashiria
uvunjifu wa haki za binadamu.”, alisema Rodriguez na kusisitiza kuwa ili
kukomesha vitendo hivyo ni kuwepo na utawala wa kisheria utakaotenda
haki kwa wale wanaoozalilishwa utu wao.
Aidha
Bw. Rodriguez aliyataka madawati ya jinsia kutumia vyombo vya habari
kuwaelimisha wananchi kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia
ili kuhakikisha vinapungua ama kuisha kabisa kwa lengo la kujenga jamii
yenye uadilifu.
Naye
Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma
alifafanua kuwa kesi za ubakaji kwa wanawake na watoto zimepungua
ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Alisema
kwa sasa kuna changamoto ya utoroshwaji na utelekezaji wa watoto kesi
ambazo kwa sasa ni nyingi lakini wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi wa
kudumu ili kuhakikisha zinapungua.
Akizitaja
changamoto zilizopo katika dawati hilo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa
ushahidi wa kina kwa baadhi ya kesi hivyo kupelekea kuharibu mwenendo
mzima wa kesi kutokana na kukosekana uthibitisho.
Mtendaji
wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji
cha Mahonda, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma akitoa taarifa
fupi ya maendeleo ya kituo hicho tangu kufunguliwa ikiwa ni mwaka mmoja
sasa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani)
ikiwa ni awamu yake ya pili kutembelea Dawati hilo. Kulia ni Mtaalamu
wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
Alifahamisha
kuwa changamoto nyingine ni jamii ya wazanzibar kuwa na tabia ya
mukhari (kuoneana haya) hivyo kumaliza kesi kwa njia ya kifamilia bila
ya kufuata utaratibu wa kisheria, hali inayokuwa kikwazo cha kuwafikisha
katika vyombo vya kisheria wahalifu wa kesi za ubakaji.
“Bado
nasisitiza ni lazima Wazanzibar tubadilike na kuondokana na masuala ya
muhari kwani unawaumiza watoto wetu na tujenge utamaduni wa kujiamini
kwa kutoa ushahidi ili tutokomeze janga hili.,” alisisitiza Fatma.
Pamoja
na hayo alishukru msaada unaoendelea kutolewa na Umoja wa mataifa (UN)
kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwawezesha katika mambo
mbali mbali kwa lengo la kupunguza vitendo vya udhalilishaji wa
kijinsia.
Mwakilishi
huyo Mkazi katika ziara hiyo alitembelea miradi mbali mbali ya umoja
huo ikiwa ni moja ya sherehe za kutimiza miaka 70 ya kuanzishwa kwa
umoja huo.
Baadhi
ya waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar na maofisa wa Umoja wa
Mataifa waliombatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(hayupo pichani) katika ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja
wa Mataifa visiwani humo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia kitabu cha orodha za
kesi katika Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika
Kijiji cha Mahonda. Kulia ni Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la
Polisi Koplo, Fatma Juma na kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi
kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa ndani ya chumba cha
dawati la Jinsia.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa Upelelezi
wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kombo Khamis
Kombo (kulia) alipofanya ziara ya kutembelea Dawati la Jinsia na Watoto,
Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu
kuanzishwa. Kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa
UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
Mradi huu ulifadhiliwa kwa pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF.
Muonekano wa jengo la Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Kaskazini Unguja.
Post a Comment